Header Ads

DC Mjema awataka Viongozi wa Kanisa la Wasabato Kurutini Mbondole kuendeleza ushirikiano kukamilisha ujenzi wao.




Mkuu wa Wilaya ya ilala, Mh: Sophia Mjema , amesema ujenzi wa Kanisa la  Wasabato Kurutini Mbondole utakamilika endapo waumini wataonyesha umoja  usio na mashaka.


Amesema hayo leo  wakati wa harambee ya ujenzi wa Kanisa la  Wasabato Kurutini Mbondole lililopo Kata ya Msongola, Wilaya ya Ilala.

Akizungumza na Waandishi wa habari, DC Mjema, amesema kama umoja waliouonesha kipindi chote mpaka sasa wapo katika hatua za ujenzi waendelee nao ili kufanisha kukamilika kwa Kanisa hilo.

 Amesema ili Maendeleo yawepo panahitajika umoja, mshikamano pamoja na usalama. Amesema anaimani kubwa kwamba ujenzi huo utakamilika ili wale waliopotea warudi katika mstari mnyoofu wenye  moyo wa kuwatumikia watu wengine.

 Aidha Amesema kuwa, Amani ndio Msingi wa Maendeleo kwamba  mahala ambapo hakuna amani  Maendeleo ni ndoto  na hayawezi kuja.

 " Nawapongeza waumini kwa kusimama imara hatimaye kufikia hatua hii, kubwa Viongozi mmepambana sana ninefarijika kuona kuna kahatua mmefikia sasa hii misaada inayotolewa hakikisheni inatumika kikamilifu katika ujenzi badala ya matumizi binafsi na familia zenu, tuwe waaminifu kama mlivyoanza naimani kila kitu kitakwenda kama mlivyopanga" Amesema DC Mjema.

 Amesema  matarajio yake ni kuona Kanisa hilo linawapiga msasa wale wote  waliopotoka kimaadili na mafisadi pamoja na wazinzi lengo likiwa ni kujenga watu wenye  mapenzi mema na Taifa lao.

Amesema licha ya Ofisi yake kuchanga , bado wataendelea kushirikiana hadi pale ujenzi utakapokamilika.

 Kuhusu miundombinu, amesema kabla ya mwezi Desemba kuisha ataleta greda  kwa ajili ya kuchonga bara bara  ili kurahisisha usafiri kwa waumini kufika vizuri na kwa wakati katika ibada.

Pia amewahakikishia kujenga Wilaya ya Kipolisi katika kata hiyo ili kuhakikisha wanaimarisha halo ya ulinzi na usalama kwa wananchi wa eneo hilo.

 Amewataka wakina mama , Vijana na walemavu kukaa vikundi vikundi katika kupatiwa mikopo kwa ajili ya kujiendeleza.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbondole, Thomas Nyanduli, amempongeza DC Mjema kwa kazi kubwa anayoifanya katika Wilaya ya Ilala pamoja na kujitoa katika mialiko mbali mbali.

 Amesema kuwa, DC Mjema amesaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha ujenzi wa daraja la  Majoe kwenda Mbondole kwa Bosco, ujenzi wa Zahanati pamoja na matundu ya choo  n.k.

Pia amesema DC Mjema amekuwa mstari wa mbrle katika kutatua migogoro ya ardhi.

" Huyu mama anafanya kazi kweli, hakuna eneo lililokuwa linatisha kwa kuongoza kwa migogoro ya ardhi kama Mbondole, lakini sasa imepungua tunampongeza sana Mungu ambariki" Amesema  Nyanduli .

 katika harambee hiyo, licha ya kuahidi Mifuko ya Saruji 30 lakini ameahidi kutoa Pesa tasilimu za kitanzania shilingi Laki 5 huku akisema panapo uhitaji wake yupo tayari kushirikiana nao.

 Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Jimbo la  Kusini Mashariki Mwa Tanzania, Mchungaji Wilfred Mafwimbo, amempongeza DC Mjema kuhudhuria katika harambee hiyo.

Amesema wapo Viongozi wangewaita lakini wamemuona DC Mjema ni kiongozi mwenye uthubutu na kushughulikia matatizo ya wananchi kwa haraka.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.