DC Mjema atoa pongezi kwa anezylitta kuendeleza sekta ya Viwanda Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya ilala, Sophia Mjema, ameipongeza Taasisi ya Anezylitta inayomilikiwa na Mwanadada Bi Zena, baada ya kuwakutanisha Wajasiriamali wa Keki pamoja.
Hayo ameyasema kwenye Jana kwenye hafla fupi ya Ukataji Keki iliyofanyika Jana kwenye ukumbi wa King Solomon Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari , DC Mjema , amesema huo ni mwanzo mzuri kwani wanaishi na kauli ya Rais John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda.
Amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha ina wabeba Wajasiriamali haswa kuwawezesha wakina mama kupitia Majukwaa ya uwezeshaji ya wanawake.
Amesema kuwa pamoja na bidhaa zao kuwa nzuri lakini wajitahidi kuhakikisha huduma zao zinakuwa nzuri na zinachukua muda mfupi baada ya wateja kuweka oda za bidhaa.
Pia amesema yupo tayari kuona Wajasiriamali hao wanawezeshwa ili kufikia ndoto zao. Amewataka wakina mama wote wajiunge kwenye Majukwaa ya wanawake ili wawe karibu na fursa.
" Tumeona bidhaa ni nzuri sana lakini zingatie muda wa kutoa huduma zenu sio oda mnachelewesha oda inatoka haraka huduma ifanyike, mkifanya hivyo mtakuwa mmejihakikishia soko na mtafanya kazi kweli kweli" Amesema DC Mjema.
Naye Mkurugenzi wa Scaba scruba, Sheikh Sharif ambaye pia ni Mjumbe wa Amani Mkoa wa Dar es Salaam,amempongeza DC Mjema kwa kazi nzuri anayoifanya katika Wilaya yake.
Amesema ujio wa DC Mjema katika hafla ya Ukataji Keki utaongeza morali ya uzalishaji wa Keki bora na kuongeza Masoko.
Pia amewataka Wajasiriamali waunge mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano za Tanzania ya Viwanda ili kuleta Maendeleo kwao na Taifa kwa Ujumla.
" Tunampongeza sana DC Mjema, kwanza kufika katika shughuli yetu hii ya Leo kwani ameacha majukumu yake kuungana na sisi , chengine uwepo wake atatuunganisha na wadau mbali mbali katika upatikanaji wa Masoko kwa kukubali kuwa mlezi wetu hilo litawezekana" Amesema Sharif Scaba Scuba.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Anezylitta, Bi Zena Mohamed, amempongeza DC Mjema hivyo amemuahidi kufika mbali zaidi kwani uwezo na nia anavyo.
Pia amemtaka DC Mjema kuwaunganisha na wateja ili Wajasiriamali hao kupata Masoko. " Hii ni ishara tosha Wajasiriamali tunapiga hatua, tunataka kuona kauli hii ya Tanzania ya Viwanda twende nayo katika kutunufaisha Wajasiriamali na kulipa kidi kwa Maendeleo ya Taifa" Amesema Zena.
Katika hafla hiyo fupi ya Ukataji Keki, kuliambatana na ugawaji wa tuzo na zawadi kwa Wajasiriamali waliofanya vizuri katika kutengeneza Keki. Mbali na ugawaji wa tuzo hizo pia hawakuwaacha washiriki mbali kwani walitoa vyeti kwa washiriki wote katika kuwatia moyo Wajasiriamali kuelekea uchumi wa Viwanda
Post a Comment