Header Ads

Dc Mjema awataka wana Ilala kutembea kifua mbele kupitia mradi wa Daraja jipya la Selander.





MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, amewataka wana Ilala kutembea kifua mbele baada ya tukio la  uwekeji Jiwe la  Msingi Leo maeneo ya AghakhanDc  Mjema awataka wana Ilala kutembea kifua mbele kupitia mradi wa Daraja jipya la  Selander.



Hayo ameyasema leo  mbele ya Rais baada ya kutambulisha  uongozi wake wa Wilaya katika ngazi zote pamoja na Viongozi vyama ikiwamo chama chenye kutekeleza Ilani CCM.


 Akizungumza na Waandishi wa habari, DC Mjema, amempongeza Rais John Magufuli, kwa wazo lake hilo ambalo litasaidia kupunguza foleni katika Jiji la  Dar es Salaam, hususani Baraba ya Alhassan Mwinyi kupitia Daraja la  Salenda.

Amesema Daraja hilo linalojengwa kwa ushirikiano wa Taifa la  Kikorea , pia litapelekea kujenga ushirikiano bora na kulitangaza Taifa letu ikiwamo Jiji la  Dar es Salaam na viunga vyake.

Pia amesema Serikali ya John Magufuli imedhamiria kuhakikisha inapunguza kero za usafiri katika Jiji la  Dar es Salaam kama ilivyo Daraja la  Mfugale na uzinduzi wa Bara bara nane  ( interchange) litakalo unganisha Ubungo hadi Kibaha.

" Hii ni fursa kwetu, tutaitangaza ilala, na Mkoa wa Dar es Salaam hivyo kukamilika kwa Daraja hilo kutasaidia sana kupunguza foleni na kuwa kivutio kikubwa cha utalii ndani ya Wilaya yetu" Amesema DC Mjema.

 Pia amesema sasa ni mwendo wa kazi hivyo kila kukichwa Rais anaota ndoto zenye kuwa kweli.

" Tunampongeza sana Rais wetu, ni mchapa kazi , Rais ambaye ana ota ndoto za kweli akilala akiamka mambo yake yanakuwa kweli sio wengine wanaota ndoto wanaziacha kwenye Godoro" Ameongeza DC Mjema.

 Pia ametoa shukrani kwa Viongozi wote pamoja na wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia uwekaji wa Jiwe la  Msingi Daraja la  Salender..


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.