Header Ads

Waziri Mbarawa awajaza furaha wakazi wa Bonyokwa.








WAZIRI wa Maji, Proffesa Makame Mbarawa, Leo amefanya ziara ya kusikiliza kero Za Maji kata ya Tabata na Bonyokwa lakini kubwa zaidi ni kupatiwa ufumbuzi wa upatikanaji wa Maji katika kata ya Bonyokwa.

 Katika ziara yake, alipata wasaa wa kusikiliza kero kwa wakazi wa Tabata pamoja na Bonyokwa huku shangwe kubwa zilizorindima ilikuwa ni kwa wakazi wa Bonyokwa Mara baada ya kuhakikishiwa wiki inayoanza kazi ya upatikanaji wa Maji inakwenda kuanza Mara moja.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika mjumuisho wa ziara yake, amesema zipo changamoto nyingi  zinazowakumba wananchi lakini nyingi  zinatokana na Watendaji wa DAWASA kutowakibika ipasavyo.

Amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha inatoa huduma ya Maji bila ya upendeleo wowote pasipo na viashiria vya ubaguzi.

Amesema ziara hizo anazozifanya zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua kero za Maji kwa wananchi.

Aidha amesema zipo taarifa baadhi ya wananchi hawasikilizwi wanapopeleka taarifa ofisi zao huku akisema kama wapo Watendaji wamechoka kazi hiyo waseme kwani watu wapo wengi wanaoweza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Kuhusu kupasuka kwa Mabomba, Waziri Mbarawa, amekiri kuwepo kwa taarifa hizo na yeye amekuwa mstari wa mbele katika kupiga picha mabomba yaliyopasuka kisha kuzituma kwenye mitandao ya kijamii ya DAWASA nakupatiwa ufumbuzi.

Amesema kila eneo mabomba yanapasuka ila shida iliyopo ni kutofanyiwa kazi dhidi ya malalamiko yanayoelekezwa kutoka kwa wananchi.

" Nikitu cha ajabu sana kuona mabomba Yanapasuka na miundombinu mibovu  lakini utakuta Watendaji wanakaa kimya, sitaki tabia hiyo kama hamuwezi kazi semeni tubadilishe watu wapo wengi, mbona Mimi nikitoa taarifa za uharibu wa mabomba haraka sana mnatatua kwanini malalamiko ya wananchi hamyafanyii kazi? Sitaki nataka mfanye kazi kama timu mhakikishe kero za Maji zinataturika Mara moja ambapo nitakaa mwezi mmoja nitarudi tena kuona " Amesema Waziri Mbarawa.

 Wakati akiwa kata ya Tabata, Waziri Mbarawa, amemtaka Meneja wa DAWASA Tabata kuhakikisha anayafanyia kazi matatizo yote zikiwamo malalamiko ya wananchi ili kero ya Maji iondoke.

Amesema DAWASA ipo  kwa ajili ya Wananchi hivyo wanatakiwa wasawazishe matatizo yao kama wanahitaji kuwatumikia wananchi.

Amesema Maji yatatoka masaa 24, huku akisema ikitokea shida kama upasukaji wa mabomba au suala la  umeme watatoa taarifa katika Vyombo vya habari na kwa Watendaji wao.

Naye Afisa Mkurugenzi DAWASA, Sprian Luhemeja, amesema kuanzia kesho tanzisha Dawati ikiwa na lengo la  kusikiliza kero zinazohusu DAWASA.

Amesema kwa kufanya hivyo watapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto za upatikanaji wa Maji Safi na salama.

Kuhusu upatikanaji wa Maji kiasi kidogo Kata ya Tabata unatokana na uzalishaji mdogo wa Maji kutoka Ruvu juu lakini wiki hii Maji yatatoka kama kawaida. Kuhusu kero ya Mtaa wa Tenge, amesema kulikuwa na Tatizo la  kuharibika kwa kizibo hivyo kutengenezaji ushafanyika na Maji yatatoka.

Katika hatua nyingine amewaomba waale wrote wenye  malalamiko juu ya shule kutopata Maji, wafike ofisini kwao wajiandikishe kama utaratibu unavyosema watapatiwa Maji.

Pia amesema upasukaji wa mabomba unatokana na presha ya Maji kuwa kubwa hivyo ubora wa mabomba ni Daraja B ( class B), ambayo hayana uwezo wa kuhimili presha hiyo. Naye mkazi wa Tabata Matumbi, Somoe Mohamed, amesema Mtaa huo hauna Maji safi na salama.

Amemuomba Waziri Mbarawa kuwasaidia kwani Maji hayo yanaweza kusababisha magonjwa ya milipuko kama vile Kichoçho pamoja na kuharisha.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.