Mbunge Zungu awataka Wanawake Ilala kuchangamkia Mikopo
MBUNGE wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu amewataka Wanawake wa Jimbo la Ilala kuchangamkia mikopo ya Serikali isiyo na riba ambayo inatolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Zungu aliyasema hayo Dar es Salam leo wakati wa kikao cha Kufunga Mwaka kinachoelezea Maendeleo ya kata ya Upanga Mashariki kilichoandaliwa na Diwani wa kata hiyo Sultan Salim
"Serikali inatoa mikopo isiyo riba,kwa watu watano watano na vikundi vilivyosajiliwa kwa Wanawake,Vijana na watu wenye Ulemavu"alisema Zungu
Aidha Zungu aliwagiza Maofisa Maendeleo wa kata zote Jimboni Ilala kuwapa semina Wananchi wake ili waweze kupata mafunzo hayo wachangamkie mikopo.
Alisema mara baada kuwapa elimu hiyo wawape fomu za usajili mara moja ili waweze kuwai hii Frusa ya fedha za Serikali.
Wakati huohuo alipongeza uongozi wa kata ya Upanga mashariki unaongozwa na Diwani Sultan kwa kupiga hatua katika Mikakati ya Maendeleo katika kipindi cha mwaka 2018/2019.
Pia aliagiza Wenyeviti wa Serikali za mtaa kushirikiana katika suala la Ulinzi Shirikishi na Wajumbe wao kila mgeni anayeingia katika Mtaa ziwekwe taarifa za kumbukumbu kwa ajili ya Usalama.
Alizitaka baa zote na kumbi kufuata taratibu za Serikali kupiga muziki kwa Sauti ya Chini bila kuwafanyia fujo watu wengine.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Upanga Mashariki Sultan Salim alisema mkutano huo wa kufunga mwa Mwaka ulikuwa ukijadili utatuzi wa Kero za Wananchi na kuwasilisha shughuli za Maendeleo.
Diwani Salim wakati akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya kata aliwaalika pia Watendaji wa Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya kutoa Elimu ,Watendaji wa MANISPAA ya Ilala walitoa elimu ya Afya.
Akizungumzia taarifa ya ulinzi na Usalama ya Kata hiyo alisema Usalama upo wa kutosha kwa kushirikiana na Polisi Jamii na jeshi la Polisi Kuanzia Septemba hadi Desemba Mtaa wa Kitonga hali ya Usalama ni nzuri vijana wa ulinzi wanafanya Doria kila siku na Mtaa wa Kibasila wameweza kudhibiti uhalifu Agosti hadi Novemba 2018 waliunda Mpango mkakati wa Ulinzi.
Alisema Mpango huo ulishirikisha ulinzi Jamii na Bodaboda 50 na ulinzi Jamii wa Kibasila Utaki Jumla yao 18 wakiongozwa na mgambo wa kata.
"Polisi Jamii waliopo kata hiyo wameweza kushirikiana na Askari wa kituo cha Polisi Salendar Bridge katika kuimalisha ulinzi "alisema Sultan.
Wakati huo huo Diwani Sultan alielezea Kero yake kwa Mbunge wa Ilala Mussa Zungu kuhusiana na Wakala wa Barabara TARURA wameshindwa kuzisimamia kutengeneza barabara za kata hiyo na kumtaka Mbunge Zungu kufatilia ili kuondoa kilio cha Wananchi wa Upanga mashariki kufuatia barabara za mtaa yao kusaulika.
Kwa upande mwingine aliwataka Wakazi wa Upanga waliokosa Vitamburisho vya TAIFA vya (NIDA) kujisajili Serikali ya Mtaa na vielelezo vyao ili taratibu za kupata vitamburisho zifanyike ambapo Mbunge wa Ilala Mussa alisema atawaleta Maofisa wa NIDA kwa ajili ya kuwafanyia uhakiki upya wakazi wa Upanga masha
Post a Comment