DAS ilala akoshwa na Utendaji wa Waziri wa Maji baada ya kero ya muda mrefu Bonyokwa kupatiwa ufumbuzi.
KATIBU Tawala wa Wilaya ya Ilala , Sheila Edward Lukuba, amesifia utendaji kazi wa Waziri wa Maji, Prof: Makame Mbarawa, baada ya kuchukua hatua maridhawa kutatua kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiikumba Kata ya Bonyokwa kutokupata Maji kwa muda mrefu.
Akizungumza na Waandishi Wa habari mapema leo Mara baada ya kukamilika kwa ziara ya Waziri Mbarawa, DAS Sheila amesema Bonyokwa ni miongoni Mwa kata ambazo zilikuwa na shida kubwa ya upatikanaji wa Maji safi na Salama ambapo kilio hicho kilikuwa kikipigiwa kelele sana na wananchi hao kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya ilala.
Amesema kero hiyo ni ya muda mrefu kwani katika Ziara ya Mkuu wa Wilaya , Mh:Sophia Mjema, ya kutembelea Kata kwa Kata katika Majimbo yote matatu ya Wilaya ya ilala, ajenda kubwa ilikuwa ni ukosekanaji wa Maji safi na salama.
Amesema wakazi wa Kata hiyo wamekuwa katika wakati mgumu wa kutembea umbali mrefu wa kutafuta Maji kiasi cha kusababisha ubakaji na vitendo vya kinyama dhidi ya Watoto.
Hata hivyo amesema katika ziara ya Mkuu wa Wilaya, tayari DC Mjema alishatoa maelekezo ya kufanya hivyo kitendo cha Waziri kufika eneo hilo ni muendelezo wa ahadi ya DC Mjema na jitihada kubwa kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea , Mh: Bonna Kaluah pamoja na Meya wa Manispaa ya Ilala, Mh: Charles Kuyeko ambaye ni Diwani wa Kata ya Bonyokwa.
" Nimefarijika sana kuona Wananchi wangu wanakwenda kuandika historia mpya ya upatikanaji wa Maji, tatizo hili lilikuwa sugu sana kiasi cha Wananchi kukosa imani na vongozi wao huku wakiamini wanapigwa siasa lakini Leo mmejionea wwnyewe ni kwa jinsi gani Serikali hii ya awamu ya tano inawajali wananchi wake, nimpongeze DC Mjema kwa kuwa kiunganishi bora katika mpango huu amepambana,Mbunge Bonna Kalua kapambana na Meya Kuyeko lakini shukrani za dhati kwa Waziri wa Maji , Prof: Mbarawa kuvunja mzizi wa fitina na hatimaye kazi inaanza hii inaonesha kwamba tupo makini na Ilani ya Chama chetu CCM inafanya yale yaliyoahidiwa kwa 95% wananchi watanufaika sana" Amesema Das Ilala.
Naye Afisa Tarafa Ukonga, Ndugu Nikodemas Shirima, amempongeza Waziri Mbarawa kwa kazi nziri ya kuwatumikia wananchi hususani katika upatikanaji wa Maji safi na Salama. Amesema Serikali ya awamu ya tano imrdhamiria kwa kiasi kikubwa kutatua kero kwa 100% hususani matatizo sugu ikiwamo suala la upatikanaji wa Maji safi na salama Mijini na pembezoni Mwa Miji.
" Huu ni utendaji wa kasi ya Rais John Magufuli , tunataka kuona ziara zikiwa na matokeo chanya kama hizi ili wananchi wapate Maendeleo na kuendelea kuwa na imani na Serikali yao" Amesema Shirima.
Hata hivyo, Waziri Mbarawa hakuishia hapo alianza ziara hiyo Kata ya Tabata na kusikiliza kero huku akitoa maelekezo kwa Watendaji wa DAWASA kutatua kero zote zinà zoletwa na Wananchi. Ziara hiyo itaendelea tena kesho, ambapo Waziri Mbarawa atatembelea Kata ya Kiwalani.
Post a Comment