Ziara ya Naibu Meya ilala yazidi kuwakuna Wajasiriamali Vingunguti
NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala, ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto, ametimiza ahadi ya Mkurugenzi ya kuwataka Madiwani wakae na wananchi wao kutoa elimu ya mikopo ikiwamo Ujasiriamali.
Hayo ameyafanya Leo huku kukiambata na zoezi la kongamano la vijana katika viwanja vya vingunguti eneo la relini kuhusu utoaji wa elimu ya
stadi za maisha,elimu rika na afya ya uzazi
, Elimu ya ujasiriamali,uundaji wa vikundi,fursa zilizopo ndani ya manispaa pamoja na Elimu ya kujitambua na kujithamini kwa vijana
Vijana wote wa manispaaa ya ilala.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema Kongamano hilo limeandaliwa na halmashauri manispaa ya ilala.
Aidha amesema atahakikisha Kata yake inafanya vizuri katika marejesho baada ya kazi ya ugawaji mikopo itakapo kamilika.
Mbali na kongamano hilo , pia amefanya muendelezo wa ziara yake ya kuwatembelea Wajasiriamali ili kubaini changamoto zinazowakumba.
" Huu ni mwendelezo wa ziara yangu ya kuzungumza na wajasiriamali ambapo nataka kuhakikisha hata fedha za mikopo za Manispaa zikitoka kata yangu iwe inaongoza kwa kufanya marejesho" Amesema kumbilamoto.
Katika hatua nyingine tulishuhudia Naibu Meya huyo akikamilisha ahadi ya kumnunulia mama Mlemavu Magogongo mapya Mara baada ya kuomba msaada kupitia kwake.
" Napenda mtambue hii ni ahadi huyu mama alinifuata lakini baada ya kujidhihirisha nikaona ipo haja ya kupatiwa magongo mapya na leo nimetimiza, natoa ushauri kwamba sio yeye anachangamoto hiyo bali wapo wengi lakini wakijitokeza tutawasaidia kadri itakavyowezekana" Ameongeza kumbilamoto.
Pia amewataka wakina mama kujituma kwani Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwawezesha na kuwanyunyua kiuchumi kupitia majukwaa yao ya uwezeshaji.
.
Post a Comment