Header Ads

DC Mjema awataka wakina mama kudumisha amani hapa nchini







MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, amewataka wakina Mama kuwa mstari Wa mbele kulinda Amani ndani na nje ya familia.

 Hayo ameyasema Leo wakati Wa Siku ya Maulidi katika kuadhimisha Mazazi ya Mtume Mohammad ( S.W.A) yaliyofanyika Upanga Jijini Dar Es Salaam, chini ya Taasisi ya Wanawake ya Kiislamu ya Neemat.

 Akizungumza mbele ya hadhara hiyo, DC Mjema,amesema duniani kote Amani ya kwanza hujengwa na wanawake.

Amesema kuwa Wanawake Wa Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla wanapaswa kutambua wanafursa kubwa hususani Katika Serikali ya awamu ya Tano imekuwa ikitengeneza imani kubwa sana juu yao ili kuweza kuzalisha kizazi chenye imani na Mungu.

 Aidha, amesema kipindi cha nyuma hata Viongozi wengi walikuwa wakipewa vyeo vikubwa in wanaume hivyo kwa sasa lazima watembee vifua mbele kwani wana Rais mwenye kuwajari na kuwapatia nafasi.

"Amani ndio kila kitu, hatuwezi kufikia malengo Kama nchi yetu haina Amani, hatuwezi kuweza kuwa na ndoto kubwa bila amani, hivyo ndugu zangu waislamu Wanawake tunawaomba mhakikishe familia zenu zinawalea watoto katika misingi ya kiroho ili tuje  kuwa na viongozi bora watakao fikisha nchii hii kujitangaza kama ilivyo sasa na kulinda sifa yetu ya amani tuliyonayo" Amesema DC Mjema.

Pia amewataka Wanawake waislamu kutengeneza umoja na mshikamano katika kufikia malengo huku akiamini Serikali yao chini ya Rais John Pombe Magufuli inawajali na kuwasikiliza.

Pia amewaomba waingia katika mifuko mbali mbali ya uwezeshwaji katika mikopo ili wanufaike katika kutimiza Sera ya Mh: Rais John Magufuli kutoka kwenye uchumi Wa chini kufikia wakati na ikiwezekana uchumi mkubwa zaidi kama Mataifa mengine yalivyopiga hatua.

Naye Katibu Wa Taasisi ya Neemat Foundation , Bibi Hadija Mzee Mwita, amesema lengo la  kufanya maulidi hayo ni pamoja na kuweza kukumbuka malengo makuu matatu aliyoyaacha Mtume Mohammad ( s.w.a) ikiwamo Umoja, Amani na Ushirikiano.

 Amesema katika ushirikiano ni kwamba dini zisibaguane dhidi ya mwenzake.

Pia katika upande Wa amani ni kwamba kuheshimu dini za watu wengine ili kulinda mipaka isiingiliwe kupitia dini ya kiislamu kwani katika amani kila binadamu yupo sawa na anahaki kulinda Amani ya mwenzake na kwa Taifa kwa ujumla.

Aidha amesema kila ifikapo madhimisho hayo ya maulidi Siku moja kabla wanakwenda kutembelea Hospitali kama walivyofanya katika Hospitali  ya Ocean Road na kutoa huduma Kama vile chakula pamoja na vifaa mbali mbali.

 Amesema maulidi hayo ni ya 12 kufanyika kila mwaka ambapo miaka yote yanafanyika Tambaza huku yakiudhuriwa na Wake Wa Viongozi mbali mbali wastaafu na Wa sasa ambapo Leo waliofika ni pamoja na Mke Wa Rais Mstaafu Wa awamu ya Pili Mama Siti Mwinyi, Mkuu Wa Wilaya ya Ilala , Mh Sophia Mjema, Mke Wa Adam Kimbisa pamoja na Mke Wa Said Kova.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.