Header Ads

JUMUIYA YA WAZAZI MKUNDI YAPONGEZWA KWA UBUNIFU WA MIRADI










MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi  CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Salum Kipira, ameipongeza Jumuiya ya Wazazi Kata ya Mkundi kwa ubunifu wa miradi ya maendeleo.

Hayo ameyazungumza katika Ufunguzi wa Baraza la Wazazi Kata ya Mkundi Desemba 31/2022.

 Kipira, amesema Jumuiya nyengine ziige mfano wa Mkundi kwani katika kipindi cha miezi michache tangu waingie madarakani washapata ekari 10 ambapo ekari 5 watatumia ujenzi wa Shule ya Chekechea na ekari 5 kwa ajili ya mradi wa ufugaji nyuki.

Kipira,  amesema kuwa Jumuiya hiyo imejipanga kuhakikisha inaendelea kuchapa kazi kwa manufaa ya jamii na chama pia.

" Nimeona mmeanza vizuri mna miradi mizuri, haya ndiyo tunayoyataka katika Jumuiya yetu, hatuhitaji Jumuiya ombaomba, itekelezeni miradi yenu vizuri ili mtimize vizuri  kaulimbiu ya Siasa na Uchumi ili kuimarisha Jumuiya na  Chama kwa ujumla" Amesema Kipira.

Katika hatua nyingine, amezitaka Jumuiya ngazi ya Kata zijipange katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na kusimamia malezi katika maeneo wanayoishi.

Mwisho, Kipira, ametoa pongezi kwa  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro, Fikiri Juma pamoja na Katibu wa Chama Amiri Mkalipa, kwa kazi nzuri wanazozifanya ya kusimamia Chama na Jumuiya zake katika kuwaletea maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Mkundi, Daudi Msuya, amesema watahkikisha miradi ambayo wameiibua inakamilika ili kuifanya Jumuiya hiyo ijiendeshe.

" Tumejipanga vizuri, ujenzi wetu wa shule ya awali tutaanza na madarasa 3 yatakayo gharimu milioni 75 na baada ya miezi 4 mbeleni tutaanza na ufugaji wa nyuki baada ya kupata semina , kwa sasa tumeanza na miradi ya muda mfupi ambayo ni sabuni na Batiki" Amesema Msuya.

 katika Baraza hilo, Mwenyekiti Kipira alipata fursa ya kuzindua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Kata ya Mkundi ikiwamo mradi wa Batiki na sabuni ya maji.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.