MWENYEKITI WAZAZI CCM KATA YA TUNGI ATOA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI WANOISHI MAZINGIRA MAGUMU.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro , Mchungaji Rev. Gabriel Chegere, ametoa msaada wa madaftari na kalamu kwa wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu wanaosoma katika shule ya Msingi Tungi na waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Tungi Estate.
Rev. Chegere, alitoa msaada huo Januari 09/2023 ambapo katika zoezi hilo la kutoa msaada ,aliambatana na Viongozi mbalimbali ikiwamo Katibu Malezi Kata ya Tungi, Blantina Chibinda, Katibu wa Wazazi Kata na Viongozi wengine wa Jumuiya ikiwamo Jumuiya ya Vijana.
Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo, amesema siyo watoto wote wazazi wao wanauwezo wa kuwanunulia vifaa vyote vya shule, na hivyo kuamua kutoa msaada wa madaftari, na kalamu, kwa wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu ili wafurahie masomo yao.
"Nimefarijika kuona hali ya uandikishaji wanafunzi katika shule zetu za Kata siyo mbaya, naomba wazazi waendelee kuleta watoto wao shuleni, elimu ni bure na hakuna ulipaji wa Ada," alisema Rev. Chegere.
Katika hatua nyengine, Rev. Chegere aliwataka wanafunzi wasome kwa bidii na kuacha utoro ili watimiza ndoto zao, wakati Serikali ikiendelea kuwaboreshea mazingira mazuri ya kusoma.
Nao baadhi wanafunzi ambao wamepewa msaada huo wa vifaa vya Shule, zikiwamo Madaftari, na Kalamu, wamempongeza Mwenyekiti wa Wazazi , Rev. Chegere , huku wakiahidi kusoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao.
Post a Comment