KAMATI YA FEDHA , UONGOZI NA MIPANGO YARIDHISHWA NA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA MOROGORO.
Pongezi hizo zimetolewa Januari 30/2023 katika ziara ya kukagua miradi hiyo ikiwamo ujenzi wa Zahanati mpya ya Kauzeni , Shule mpya ya Msingi Kihonda Maghorofani pamoja na Ujenzi wa Jengo la Utawala shule ya Sekondari Mkundi.
Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo, Mh. Kihanga, amepongeza Menejimenti na Watendaji kwa kusimamia kikamilifu miradi hiyo ya maendeleo ambayo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani.
Mhe, Kihanga, amesema kwamba kiujumla miradi imetekelezwa kwa kiwango na ubora na thamani ya fedha inaonekana ambapo katika mradi wa ujenzi wa Zahati ya Kauzeni ujenzi unatarajia kukamilika Februari 25/ 2023, huku ujenzi wa Shule ya Msingi Kihonda Maghorofani ukitarajia kutumia Milioni 250 kutoka Serikali Kuu pamoja na Jengo la Utawala Mkundi Sekondari lenye thamani ya takribani milioni 98.
"Tumekagua miradi hii ambayo inaendelea , hatua iliyofikiwa miradi hii ni nzuri na ya kuridhisha, inayoonesha mwelekeo wa dhamira ya dhati ya utekelezaji na ukamilishaji wake ili kutoa huduma bora kwa wananchi, raia yangu miradi hii ikamailike kwa wakati ili ianze kutoa huduma "Amesema Kihanga.
Aidha, Mhe. Kihanga, amesema kwa ujenzi unaoendelea katika Shule ya Msingi Kihonda Maghorofani upo katika hatua nzuri na inaridhisha na kuwataka wasimamizi wa Shule hiyo waendelee kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maelekezo wanayopewa na wataalamu ili kufanya kazi nzuri na yenye viwango bora vinavyotakiwa katika ujenzi.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amesema kwa kushirikiana na Menejimenti ataendelea kusimamia kwa uadilifu mkubwa na kuhakikisha miradi maendeleo yote inakamilika ili wananchi waweze kupata huduma bora inayostahili kwa wakati.
Post a Comment