MANISPAA YA MOROGORO YAWASHIKA MKONO WAHANGA WA UKATILI WA KIJINSIA KIEGEA STAR CITY
Tukio hilo limefanyika Januari 23/2022 wakati wa Afisa huyo akiambatana na timu ya wataalamu wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi walipokwenda kuwajulia hali wahanga wa matukio hayo.
Akizungumza na wenyeji ambao wamewafadhili wahanga hao, Maduhu ,amesema suala la ukatili ni suala la kupigiwa vita kubwa hivyo upande wa Manispaa umesikitishwa na vitendo hivyo vya ukatili.
"Tumefika hapa tukimwakilisha Mkurugenzi wetu wa Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kuangalia hali ya wahanga wa matukio haya, lakini pia tumeona tulete hitaji la chakula, tumeleta unga Kg. 25 ili katika kipindi hiki cha mpito familia iweze kupata hitaji hilo, naomba kama wapo wadau wataguswa na hili pia wasisite kutoa msaada kwani bado wahanga hawa hawajapata makazi ya kudumu ya kuishi" Amesema Maduhu.
Naye Afisa Ustawi wa Manispaa ya Morogoro , Sidna Mathias, amesema wataendelea kutoa zaidi elimu ya ukatili kwani bado vitendo hivyo vimekuwa vikijitokeza licha ya elimu kutolewa.
" Naamini watuhumiwa wa kesi hii sheria itafuata mkondo, kikubwa tuwaamini wenye mamlaka, haki ya mtu haipotei , sisi upande wetu tutaendelea kutoa elimu na niwaombe wananchi tufichue matukio haya tusiyafumbie macho, tukikaa nayo yanatuumiza sisi wenyewe" Amesema Sidna.
Wahanga wa ukatili wa kijinsia ni pamoja na Bahati Katiko Kalokozi ambaye ni mume aliyejeruhiwa na mkewe Lupi Daniel Kasyupa aliyefanyiwa ukatili wa kulawitiwa na watuhumiwa washafikishwa katika vyombo vya sheria na familia hiyo imehifadhiwa kwa wasamalia wema.
Post a Comment