MANISPAA YA MOROGORO KUTEKELEZA MRADI WA BOOST KUBORESHA SEKTA YA ELIMU KIPINDI CHA MIAKA 5.
MANISPAA ya Morogoro kutekeleza mradi Boost ili kuboresha upatikanaji fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi.
Kauli hiyo imetolewa Januari 11/2023 na Mratibu wa Boost Manispaa ya Morogoro, Stephen Mkulia, katika kikao kilicho wakutanisha Wajumbe wa Boost, Maafisa Elimu Kata na Waalimu wa Kuu wa Shule za Msingi.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkulia, amesema Boost ni sehemu ya Mpango wa Lipa kulingana na Matokeo katika elimu awamu ya pili (EPforRII) na inachangia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu wa miaka mitano 2020/2021 hadi 2025/2026.
Mkulia, amesema kuwa, mradi
huo utasaidia katika ujenzi wa miundombinu kama vile madarasa na vyoo pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu ili kuwaongezea uwezo
wa ufundishaji na ujifunzaji katika shule zao.
"Tupo hapa kupeana somo juu ya mradi huu wa BOOST, malengo ya mradi huu ni kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji, kuboresha ujuzi wa waalimu na ubora wa ufundishaji darasani,kuandaa mazingira wezeshi na ya kuvutia kwa watoto wa elimu ya Awali, kuhakikisha kuwa mtoto anakuwa na mwendelezo wa kusoma darasa la Awali, " Amesema Mkulia.
Naye Afisa Elimu Kata ya Kilakala, ambaye ni miongoni mwa Maafisa elimu waliohudhuria katika mkutano huo, Thecla Mbiki, ameipongeza Serikali kwa kuja na mpango wa mradi BOOST huku akisema mradi huo utaongeza chachu ya ufundishaji sambamba na viwango vya ufaulu katika shule zao.
Mradi wa BOOST ni matokeo ya ufadhili wa watu wa Marekani, ambao unagharimu takribani dola za Marekani milioni 20 ambazo hutumika katika kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji, kuboresha ujuzi kwa wa walimu na elimu ubora wa ufundishaji darasani sanjari na kuimarisha utoaji wa fedha za ugatuzi wa huduma.
Post a Comment