JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA MOROGORO MJINI YAMPA TANO DIWANI KATA YA MZINGA.
JUMUIYA ya Wazazi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, imempongeza Diwani wa Kata ya Mzinga, Mhe. Salum Chunga, kwa kazi kubwa ya kusimamia miradi ya maendeleo hususani katika kutatua changamoto za afya na elimu.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Elimu Malezi na Mazingira, Ndg. Godwin Malambiti wakati wa ziara ya Kamati ya elimu na Malezi ya kukagua miradi ya elimu na afya inayotekelezwa Kata ya Mzinga.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mlambiti, amempongeza Mhe. Chunga, kwa kutatua changamoto ya afya na elimu huku akisema kuwa diwani huyo amekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha ujenzi wa Shule ya Msingi Konga na kuwaondolea kero ya kutembea umbali mrefu waaafunzi kutoka Konga hadi Kauzeni ambapo awali wanafunzi hao walikuwa wakisoma huko .
Mlambiti ,pia amempongeza Mhe.Chunga kwa kushirikiana na Uongozi wa CCM Kata ya Mazinga pamoja na Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa na Watendaji kwa kushiriki kuhimiza wazazi kuwapeleka watoto shule na kufuatilia maendeleo yao.
Katika hatua nyengine, Mlambiti, ametoa salamu za Wazazi Wilaya na kuwaambia Mwenyekiti wa Wazazi Salum Kipira na Katibu Ruth Mutashaba wapo pamoja na Jumuiya hiyo hivyo kila kiongozi afanye kazi kwa nafasi yake ili kuisongesha Jumuiya mbele kimaendeleo.
Mwisho, amewashauri wananchi na wadau wa maendeleo katika Kata hiyo kuendelea kuheshimu na kuthamini juhudi zinazoendelea kufanywa na diwani wao katika kuwaletea maendeleo.
Upande wa Mjumbe wa Kamati ya Elimu na Malezi CCM Wilaya ambaye pia ni Katibu Malezi Kata ya Tungi, Blantina Chibinda, amesema wazazi wanajukumu la kusimamia maendeleo hususani katika Sekta ya elimu na afya.
" Tupo hapa kuiwakilisha Jumuiya yetu, huu ni mwanzo, kamati yetu itafanya ziara kadri tutakavyoweza kujipanga, Tunashukuru Serikali kwa kutekeleza miradi hii, sisi kama wazazi tutasimama na Serikali na kumsemea Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anazofanya hususani katika Sekta ya Elimu na Afya" Amesema Blantina.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mzinga, Mhe. aliwashukuru viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM pamoja na Chama Cha Mapinduzi Kata ya Mzinga na wananchi wa Kata ya Mzinga, kwa pongezi walizompatia juu ya kazi kubwa anayoifanya ya kutatua changamoto zilizopo katika kata hiyo kwa muda mrefu.
"Mimi binafsi nimepokea pongezi hizi kwa moyo mkunjufu kwa kuwa bila ya mshikamano wetu, sisi kama viongozi, hatuwezi kufanikisha masuala ya kimaendeleo bila ushirikiano wenu "Amesema Mhe. Chunga.
Katika ziara hiyo, Katibu Malezi aliongozana na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Aman Tumbo maarufu Ndevu Nyekundu.
Zahanati ya Konga ishaingiziwa Milioni 50 na Manispaa ya Morogoro.
Post a Comment