Header Ads

JUMUIYA YA WAZAZI CCM KATA YA TUNGI IWE MFANO WA KATA NYENGINE-ZUBERI MTELELA KATIBU WAZAZI MKOA MOROGORO

KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi CCM  Mkoa wa Morogoro, Zuberi  Mtelela, amezitaka Kata nyengine pamoja na Jumuiya za Wazazi Wilaya  kuiga mfano wa Kata ya Tungi Wilaya ya Morogoro Mjini kwa kutekeleza haraka agizo la ngazi ya Kitaifa ya Chama  katika kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM ya kutimiza miaka 46.

Kauli hiyo, ameitoa Januari 23/2023 katika uzinduzi wa zoezi la upandaji wa miti 2000 katika Taasisi za Serikali ikiwemo shule ya Msingi Tungi, Shule ya Msingi Tubuyu, Shule ya Sekondari Tungi pamoja na Zahanati ya Kata ya Tungi.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha uzinduzi huo , Mtelela, amezitaka  Jumuya za Wazazi zote ndani ya Mkoa wa Morogoro kuiga mfano wa Tungi huku akitoa pongezi kubwa kwa Mwenyekiti wa Wazazi Tungi,Rev. Gabriel Chegere  pamoja Uongozi wa Wazazi Wilaya kwa kuweza kufanya tukio kubwa la kihistoria katika kuelekea miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM.

Mtelela ,amesema  upandaji miti ni jambo lisilokwepeka kwani huzalisha hewa ya oksijeni ambayo ni muhimu Sana kwa maisha ya binadamu.

Mwisho Mtelela, ametoa rai kwa Jumuiya za Wazazi  zingine kupanda miti kwa wingi hasa wakati huu wa Mvua ili kuifanya Tanzania kuwa ya kijani.

Naye, Katibu Elimu na Malezi Mkoa wa Morogoro, Ndg. Alexander Mapunda, ameipongeza Kata ya Tungi huku akisema kama Mkoa watahakikisha wanatembelea Wilaya zote kuhamasisha upandaji wa Miti.

Upande wa Mwenyekiti  wa Wazazi Wilaya ya Morogoro , Salum Kipira, ameipongeza Jumuiya ya Wazazi Kata ya Tungi huku akisema upande wa Wilaya watazindua zoezi hilo katika mradi wa Bwawa la Samaki Mzinga na kumalizia na Mkutano wa hadhara utakaofanyika Kata ya Mwembesongo siku ya tarehe 28/1/12023.

Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Tungi, Rev. Gabriel Chegere, amesema Kata ya Tungi wataendelea kupanda miti mingi lakini pia kusimamia malezi na maadili, Mazingira , Afya pamoja na masuala ya elimu.

Zoezi hilo la upandaji wa Miti lilihudhuriwa na Katibu wa Wazazi Mkoa wa Morogoro ambaye ndiye mgeni rasmi, Katibu Elimu Malezi wa Mkoa, Ndg. Alexabder Mapunda, Baadhi ya wajumbe wa Baraza  la Wazazi Mkoa, Viongozi wa Wazazi Wilaya ya Morogoro Mjini wakiongozwa na Mwenyekiti wake, CDE. Salum Kipira, Wajumbe wa kamati ndogo za Wazazi Wilaya, Baadhi ya Viongozi wa Wazazi kutoka Kata mbalimbali pamoja na Viongozi wa Chama na Jumuiya Kata ya Tungi kwa kuhsirikiana na Viongozi wa Serikali .

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.