JUMUIYA YA WAZAZI CCM KATA YA MAFIGA YAMPONGEZA DIWANI KWA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAENDELEO.
JUMUIYA ya Wazazi CCM Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro wamempongeza Diwani wa Kata ya Mafiga Mhe. Thomas Butabile kwa kazi nzuri ya kusimamia miradi ya Maendeleo.
Pongezi hizo zimeongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Mafiga, Kata ya Mafiga, Ndg. Rajabu Omary Septemba 24/2021 katika ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo Kata ya Mafiga .
Akizungumza na Wajumbe wa Jumuiya hiyo,Rajabu amesema kuwa Diwani anafanya kile Wananchi walichomtuma na kutekeleza vyema Ilani ya CCM.
" Diwani wetu mchapa kazi, nampongeza Sana kwa usimamizi wake lakini pia wataalamu wetu wa Manispaa na Kata na Wenyeviti wote wamefanya kazi kubwa kilichopo ni kuhakikisha kwamba tunailinda miradi hii kikamilifu ili iendeleee kuwahudumia Wananchi" Amesema Rajabu.
Aidha, amewataka Wananchi wa Kata ya Mafiga waendelee kumuunga mkono Diwani kwani maendeleo makubwa yanatokana na nguvu za Serikali na Wananchi.
Pia ameupongeza miradi yote na kuiomba Serikali iendeleee kusaidia katika Maeneo mengine yenye uhitaji.
" Kesho Septemba 25/2021, tuna Mkutano wetu wa Jumuiya, katika Hilo tulimuomba Mhe. Diwani atupitishe katika miradi ili tupate sehemu ya kukisemea chama na kuona utekelezaji wa Ilani, miradi mizuri na thamani ya pesa imeonekana, tunampongeza Sana Diwani na wasaidizi wake , sisi tunaahidi tutashirikiana naye kikamilifu kuona Kata yetu inafikia malengo na Wananchi wanapata huduma bora" Ameongeza Rajabu .
Naye Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe Thomas Butabile, ameishukuru Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Mafiga kwa ziara zao .
Butabile, amesema kuwa ataendelea kusimamia kikamilifu fedha za miradi zinazotolewa na Manispaa pamoja na nguvu za Wananchi ili ziwe na matunda.
" Tumefanya ziara na wenyewe Ilani wamejionea kwa kipindi kifupi yapo mambo ya kujivunia, niwaombe Sana Chama na Wananchi waendelee kutuunga mkono ili kazi iendeleee" Amesema Butabile.
Hata hivyo, .... amesema wataendeleaa Mkono Diwani na kuwa mstari wa mbele katika kufuatilia miradi iliyopo na ijayo.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa leo na Jumuiya ya Wazazi CCM pamoja na Maabara ya Kituo Cha afya Mafiga, ujenzi wa Madarasa 4 na Ofisi za Waalimu Shule za Msingi Misufini B na Mafiga A, Ujenzi wa Madarasa 3 Shule ya Sekondari Mafiga na Jengo la Utawala, na ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Kata Mafiga.
Post a Comment