Header Ads

DIWANI KANGA ATAJA MIKAKATI YA KUNYANYUA VIWANGO VYA UFAULU KWA WANAFUNZI KATÀ YA KILAKALA MANISPAA YA MOROGORO.













DIWANI wa Kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro, Mhe. Marco Kanga, ametaja mikakati maalumu ambayo itasaidia kunyanyua viwango vya ufaulu katika Kata ya Kilakala.

Mikakati hiyo amiitaja Agosti 30/2021 wakati akizungumza na Waalimu wa shule ya Sekondari Kingalu pamoja na viongozi wa Kata hiyo ikiwa ni maandalizi ya mitihani kwa madarasa yenye mitihani ya Taifa.

Akizungumza na Waalimu, Wazazi  na viongozi waliohudhuruia katika kikao hicho, Mhe. Kanga, amesema ili viwango vya ufaulu viongezeke katika Kata hiyo lazima kuwe na mikakati madhubuti itakayoweza kutumika ili kuongeza ufalu.

Mhe. Kanga, amesema katika kunyanyua viwango vya ufaulu, ameanza na mpango wa kuwaweka kambi wanafunzi wa vidato vya nne katika Shule ya Sekondari Kingalu pamoja na Lupanga jambo ambalo limeungwa mkono na wananchi wengi pamoja na wazazi wa wanafunzi hao katika Kata hiyo.

"Mpango wetu wa kambi wa siku 72 utatupa mwanya mzui wa kuwajenga wanafunzi wetu, tunaamini mpango huu utatuvusha kutoka tulipo na kwenda tunapopataka, kikubwa naomba ushirikiano wa wananchi, Wazazi , viongozi pamoja na wadau ili kuweza kufanikisha mpango huu" Amesema Mhe. Kanga.

Katika hatua nyengine amesema mpaka sasa jumla ya mbao 600 zimeshachanwa kupitia misitu yao ambayo itasadia kutengeneza zaidi ya madawati 400 na kuondoa changamoto ya madawati katika shule za Kilakala.

Mbali na hayo, amesema katika bajeti ya mwaka 2021/2022 wanatarajia kujenga jumla ya madarasa 10 ambayo yatatumika mwaka kwa wanafunzi watakao faulu kwenda kidato cha kwanza.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.