Header Ads

Mwenge Wa Uhuru wazindua miradi yenye thamani ya Bilioni 14.4 Wilaya ya Kigamboni.



Miradi Mitano  yenye thamani ya Shilingi 14.4 bilioni imezinduliwa leo wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Kigamboni jijini hapa.

Akizungumza leo Julai 23/ 2019 mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri,  amesema miradi hiyo imezinduliwa na Kiongozi Wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali ikiwa na lengo la kuchochea Maendeleo.

Amesema katika maeneo hayo, mradi mitatu imezinduliwa huku miradi miwili ikikaguliwa.


Mwenge huo uliokuwa wilaya ya Temeke   umekabidhiwa leo na mkuu wa wilaya hiyo, Mh Felix Lyaniva.

Miongoni Mwa miradi iliyozinduliwa ni pamoja na Shule ya Msingi Vijibweni miradi Wa vyumba 2 vya madarasa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 40 kutoka Serikali kuu, miradi Wa Ujenzi Wa kutolea huduma za Mionzi katika Hospitali ya Vijibweni  uliogharimu jumla ya Shilingi Milioni 101 mkopo kutoka mfuko Wa Taifa Wa Bima ya Afya NHIF, Mradi wa  Vifungashio katika Kampuni ya Isigna iliyopo Kibada wenye kugharimu Bilioni 10 fedha ya Ujenzi pamoja na vifaa Pamoja na miradi Wa Chuo cha fya  cha Kigamboni City College of health & Allied wenye vyumba 16 uliogharimu Shilingi Bilioni 3.158.

Aidha, kwa upande Wa Kiongozi Wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali, amesema miradi hiyo iwe  endelevu kwa ajili ya Wananchi.


Pia amewataka watendaji kuwa waadilifu kazini na kuachana na vitendo viovu vita kavyo pelekea kuitia doa  Serikali ya awamu ya tano. Hata hivyo ipo  miradi iliyotembelewa kama vile eneo la  utengenezaji Sofa , ufufuaji Wa bustani, miradi Wa Maji Dawasa uliopo geza ulole wenye gharama ya Shilingi 154 ambapo Milioni 3 zimetoka Halmashauri kwa ajili ya ufufuaji Wa bustani. Miradi huo Wa Maji Gezaulole unatarajia kuwanufaisha Wananchi 800 baada ya kukamilika.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.