Header Ads

Mbunge Jimbo la Segerea afanya ziara kukagua mradi Wa Machinjio Vingunguti







Dar es Salaam. Injinia Elisante Ulomi kutoka Shirika la Nyumba amesema mradi wa ujenzi wa machinjio Vingunguti unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18.

Pia utagharimu jumla ya Sh 12.47 bilioni na utakuwa na kwamba  uwezo wa kuchinja Ng'ombe 1000 na Mbuzi 500 kwa siku.

Kuhusu machinjio iliyopo kwa sasa alisema inauwezo wa kuchinja ng'ombe takribani 500 nabuzi 400 kwa siku.

Injinia Ulomi aliyaeleza hayo Leo Julai 24 mbele ya Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kamoli wakati alipokuwa akikagua mradi huo kama sehemu ya ziara yake ya siku 15.

 " Mradi huu tumekabidhiwa Juni  26, mwaka huu na tunaahidi tutahakikisha unakamilika ndani ya miezi 18 na ndani ya gharama iliyopangwa"alisema Injinia Ulomi.

Alibainisha kuwa sehemu kubwa ya wafanyakazi wa mradi huo watatoka Vingunguti na wamekwisha pokea maombi ya wakazi hao 450 mpaka sasa wakiwamo mafundi selemara na mafundi ujenzi.

Aliongeza kuwa machinjio hiyo mpya utakuwa na mfumo wa majitaka, majokofu ya kuhifadhia nyama ambayo yatakuwa na uwezo wa kuitunza hata ukiisafirisha nje ya nchi.

Hata hivyo alimpongeza rais John Magufuli kwa kuhakikisha miradi inajengwa na watanzania kwenye utaalam na siyo raia wa nje.

Kamoli akiwa katika mkutano wa ndani na mabalozi wa CCM na wenyeviti wa mashina Vingunguti alipokea kero mbalimbali.

Ambapo Salumu Matola kwa niaba ya Mwananchi wa Vingunguti alilalamikia zuio la kutoa mwili wa mtu aliyefariki hospitali kutokana na ndugu kushindwa kulipa gharama wanazodaiwa.

Akijibu kero hiyo,Kamoli alisema hilo si jambo jema hawaliungi mkono na wamekwisha peleka maoni serikali ni na kwa sasa wa nasubiri majibu .

Kuhusu maji safi Kamoli alikili Kata ya Vingunguti kuna sehemu Hazina maji na kwamba Kazi ya kusambaza maji inafanywa sasa na ifikapo Desemba mwaka huu maji  yatakuwa yanatoka.

Kuhusu barabara alikili jumbo la Segerea nyingine mbovu ukiondoa Kata ya Kiwalani na Minazi Mirefu kwa sasa hatuwezi kufanya chochote kwa sababu kuna mradi mpya unakuja na kuomba wananchi wawe wavumilivu, tusubiri.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.