Header Ads

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA BILION 13 ILALA


,

MWENGE wa  UHURU unatarajia kuzindua miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 13  wilayani Ilala Julai 19 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema alisema Mwenge mwaka huu utapokewa ukitokea Zanzibar Uwanja wa Julius Nyerere saa mbili asubuhi utakimbizwa katika wilaya tano za Mkoa wa Dar es Salaam.

"Mwaka huu mwenge utazindua miradi  ya Maendeleo  yenye thamani ya shilingi bilioni 13 katika wilaya yangu  naomba wananchi wote wana Ilala mjitokeze kwa wingi  "alisema Mjema.

Mjema alitaja baadhi ya miradi hiyo ambayo itazinduliwa hospitali ya Wilaya Kivule kuweka jiwe la Msingi,uzinduzi wa Miradi ya Vijana ya Kilimo eneo la Kitunda,mradi wa maji wa Dawasa  shule ya msingi Pugu ,hospitali binafsi Gongolamboto,Makumbusho ya Taifa Pugu nyumbani kwa Mwalimu Nyerere,choo cha Mtoto wa Kike shule  ya Msingi Ilala.

Mjema alisema  mwenge wa Uhuru mwaka umebeba kauli mbiu isemayo  Maji ni Haki ya Kila mtu ,tutunze vyanzo vyake na Tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa"

Aidha alisema pamoja na kauli mbiu hiyo mwenge wa uhuru umebeba ujumbe wa kudumu VVu /UKIMWI chini ya kauli mbiu isemayo pima jitambue ishi,nipo tayari kutokomeza Malaria wewe je? tujenge maisha yetu ,jamii yetu na utu wetu bila dawa za kulevya na ujumbe mwingine uwekezaji katika miundombinu ya maji na utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa maendeleo ya Taifa letu.

Pia Sophia Mjema alisema Mwenge huo mwaka huu utakesha eneo la Vingunguti nyuma ya Zahanati,  miradi itakayozinduliwa eneo hilo Utoji mikopo awamu ya tatu ,uzinduzi wa magari mapya ya takataka ya halmashauri ya Ilala


Miradi mingine maonyesho ya mapambano ya dawa za kulevya,maonyesho ya mapambano dhidhi ya malaria ,mapambano dhidhi ya Rushwa,maonyesho ya mapambano dhidi ya VVu/UKIMWI .


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.