Mtendaji Kata ya Liwiti awataka Wananchi kuwataja Waharifu ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Mtendaji Kata ya Liwiti Ignas Mayembe, amewataka wananchi kuwataja waharifu wote na magenge yao ili wakamatwe na wafikishwe katika vyombo vya sheria. Hayo ameyasema jana kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama kilichofanyika Mtaa wa Mfaume leo Julai 6/2019.
Akizungumza na Wananchi hayo, amesema Liwiti inamatukio mengi ya uharifu hivyo hali ya Usalama kwa kata ya Liwiti hauridhishi.
Amesema kila Mwananchi kushiriki ulinzi wa umma , hivyo amesema lazima wananchi washirikiane na Jeshi la polisi ili kupunguza na kutokomeza uharifu.
Amesema sasa ni muda wa kupangiana mikakati ili kupunguza uharifu. Amesema ifike wakati tujitahidi kuchangia ulinzi shirikishi pamoja na kutoa taarifa za uharifu.
Mtendaji amesema, Mtaa wa mfaume kata ya Liwiti , umekuwa ukikabiriwa sana na changamoto ya ulinzi na Usalama, huku akienda mbali zaidi akimtaja kijana mmoja anayejulikana kwa jina la hamadi Maarufu kwa jina la mzungu kichaa amekuwa akiwasumbua sana wananchi kwa kufanya matendo ya kiuharifu.
" Niwaombe Wananchi kuweni na amani nimepata taarifa kwamba Kijana huyo akikamatwa hutolewa , lakini nataka kuwaambieni kutolewa kwake kuna tokana na sisi wananchi kuogopa kushika dhamana la kesi pamoja na kutopeleka vielelezo vya ushahidi polisi ili mtuhumiwa akifikishwa Mahakamani achukuliwe hatua kali zaidi za kisheria" Amesema Mtendaji.
Aidha Mkuu wa kituo cha polisi Kata ya Tabata , Riziki Makwaya: amesema hiki ni kikao chake cha kwanza kata ya Liwiti ndani ya miezi saba tangia aingie kikazi.
Amesema Liwiti inamatukio mengi ya uharifu hivyo hali ya Usalama kwa kata ya Liwiti hauridhishi.

Post a Comment