DC Mjema afungua mafunzo ya kozi ya awali ya Jeshi la Akiba Wilaya ya Ilala 2019.
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema , leo Julai 3, 2019 amefungua Mafunzo ya kozi ya awali ya Jeshi la Akiba yatakayo dumu kwa miezi
Mafunzo hayo yamefunguliwa Leo kwenye Shule ya Msingi Mivinjeni iliyopo Kata ya Ilala.
Akizungumza na Waandishi wa Habari , amesema kuwa matarajio yake ni Kuona Vijana hao baada ya Mafunzo wanakuwa Wazalendo, nidhamu pamoja na Uadilifu.
Amelitaka Jeshi la Akiba kuwa Wazalendo na waadilifu kwani ikitokea Vita wao wanakuwa mstari wa mbele katika kulitetea Taifa. Pia amewataka kuhakikisha wanalinda Amani ya nchi hii ili kuendelea kuwa Taifa lenye utulivu Ulimwenguni.
Amewaasa Vijana hao Mara baada ya kumaliza Mafunzo yao wasitoe siri za ndani ya Jeshi kwani kufanya Hivyo kunaongeza uharifu mitaani.
Amewataka Vijana hao kututumika vibaya na Wanasiasa katika kuelekea uchaguzi Mkuu kwa lengo la kuleta machafuko.
" Nyinyi Vijana Taifa hili linawategemea sana, msitoe siri za ndani ya Jeshi lenu kwani Mafunzo mnayofundishwa ni ya kwenu na kumsaidia Jemedari wenu Mh Dkt John Pombe Magufuli kwa ajili ya kuendelea kulinda Amani katika nchi yetu, hatutegemei kwamba Mafunzo haya mtayatoa mtaani , mkiulizwa mmefundishwa nini semeni hatujui sawa"Amesema DC Mjema.
Aidha amesema kuwa Jeshi lina adhabu yake , hivyo wakitoa siri za ndani wataadhibiwa kama Mwana Jeshi. Aidha amewaomba Vijana hao kutoa taarifa juu ya Wahamiaji mitaani kwani wakiwepo wanapelekea kutoa Mafunzo kwa vijana kwa ajili ya kufanya uharifu.
Post a Comment