Header Ads

Kaimu Meya Ilala awataka Wana CCM kudumisha Umoja na Mshikamano kuelekea Uchaguzi Serikali za Mitaa.



KAIMU Meya wa Ilala na Diwani Kata ya Vingunguti, Mh Omary Kumbilamoto, amewataka Wana CCM kuendelea kudumisha Mshikamano na Umoja katika kuelekea Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa.

Hayo ameyasema Leo wakati wa kufungua Baraza la  Kata U.W.T Kata ya Dunda Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Leo Julai 26/2019.

Akizungumza na Wanachama hao wa U.W.T Kata ya Dunda, amesema kuwa upinzani umekufa lakini kinachoisumbua CCM ni upinzani uliopo ndani ya Chama hicho.

Aidha, ameupongeza Uongozi wa U.W.T Kata ya Dunda kwa kuimarisha Chama huku akisema upinzani Mkoa wa Dar Es Salaam umekwisha kilichobakia ni kazi tu.

Amewataka Viongozi  kufanya kazi kwa bidii ili kufikia Uchaguzi Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu njia ya ushindi iwe nyeupe.

" Niwapongeze kwa kufanya kazi, lakini tutumie fursa zilizopo  kwa Umoja wetu ili tujipatie Maendeleo " Amesema Kumbilamoto.

Hata hivyo, amewataka wana CCM kuhakikisha wanamuweka mgombea mwenye  sifa na wanaokubalika na sio kuwabeba watu wasio na uwezo watakao sababisha Uchaguzi kuwa mgumu na kushindwa kuwatangaza .


 Aidha amewaomba Wana CCM kuhakikisha wanaendelea kudumisha ushirikiano wao na Umoja ili kukiletea Chama cha Mapinduzi CCM  ushindi katika Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Naye Diwani Viti Maalumu , Mh Sumina Sharifu, amesema Wilaya ya Bagamoyo inaongoza kwa kupata mikopo.

Amesema jumla ya Shilingi Milioni 152 zimetolewa kwa Vikundi 31 ambapo vikundi 17 Wakina Mama na Vikundi 14 Vijana na Walemavu.


Kwa upande wa Katibu wa U.W.T Kata ya Dunda, Saada Kilemba, amesema Wilaya ya Bagamoyo kina kata 11 na Vitongoji 16 ambapo Vutongoji 15 vinaongozwa na CCM na Kitongoji 1 kinsongozwa na CUF kwa mujibu wa Taarifa ya mwaka mmoja na nusu Mwaka 2017-2019.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.