Header Ads

Kaimu Meya Ilala atoa Jezi na Mpira Timu ya Big Stone ya Vingunguti.




KAIMU Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani Wa Kata ya Vingunguti, Mh Omary Kumbilamoto, ametoa Jezi Seti moja pamoja na Mpira  mmoja kwa Timu ya Big Stone.


Zoezi hilo  la utoaji Wa Jezi na Mpira umefanyika leo  kwenye  Mtaa Wa Kombo Kata ya Vingunguti Julai 25/2019.

Akizungumza na Wananchi, Kumbilamoto, amesema lengo la  kutoa Vifaa hivyo vya Michezo ni pamoja na kuamsha hari ya Michezo katika Kata ya Vingunguti.

Amesema kwa kutambua Michezo ni ajira ameona kutoa vifaa hivyo vitapelekea kuleta umoja na mshikamano baina ya Wakazi Wa Kombo hususani wapenda Michezo.

Aidha amesema hiyo ni ahadi ambayo aliihaidi kipindi cha Kampeni yake .

Amesema kazi ya Kiongozi ni kuwatumikia Wananchi hivyo ahadi yake  imetimia na kilichobakia ni vijana kucheza Mpira.

" Ujio wangu ni kurudisha shukrani kwenu baada ya kunipokea wakati natoka Upinzani kujiunga na CCM" amesema Kumbilamoto.

Amesema ataendelea kutoa ushirikiano kwa Vijana hao.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.