Header Ads

Mwenge Wa uhuru Temeke wazindua Miradi yenye thamani ya Bilioni 3.7
















MWENGE wa  UHURU Wilaya ya Temeke umezindua  miradi yenye thamani ya shilingi bilioni  Julai 22 /2019 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo, Kiongozi Wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali, amesema kuwa lengo la Mwenge mwaka huu ni kuona thamani ya fedha inatumika vizuri kwani pesa hizo ni za Wananchi hivyo lazima zielekezwe katika miradi husika.

Aidha ,amesema Serikali ya Awamu ya tank imedhamiria kuhakikisha Wananchi wanapatiwa huduma ikiwamo Afya, Bara bara, Elimu pamoja na kuwezeshwa kiuchumi kwa Vijana, Wanawake na Walemavu katika 10%.

" Hii ni miradi ambayo tunatumia pesa za Wananchi hivyo lazima tuilinde na kuitunza, sisi lengo letu kuangalia ubora pamoja na matumizi yanayoendana na thamani ya pesa katika miradi hii, hivyo niwaombe hizi changamoto ndogo ndogo mkakae na kuzifanyia kazi" Amesema Mkongea Ali.

Naye Mkuu Wa Wilaya ya Temeke, Mh Felix Lyaniva, amemshukuru Kiongozi Wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali, kwa kupitisha miradi hiyo licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo.

Amesema Wilaya yake  imejipanga katika Kuona inawatumikia Wananchi wake na kuwapa huduma bora zinazostahiki ili kila Mwananchi aweze kuendelea kupata huduma ikiwamo Maji, Elimu, bars bars pamoja na Mikopo.

"Nimefurahi sana pia ni mpongeze sana Kiingozi wa mbio za mwenge Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali, changamoto zilizojitokeza tunakwenda kuzifanyia kazi, Mwaka huu mwenge utazindua miradi  ya Maendeleo  yenye thamani ya shilingi bilioni 3 katika wilaya yangu  naomba wananchi wote muilinde miradi hii ili iwe  endelevu kwa matumizi" Amesema DC Lyaniva.

DC Lyaniva ametaja baadhi ya miradi hiyo ambayo ilizinduliwa na Mbio za Mwenge Kitaifa , miongoni Mwa miradi hiyo ni pamoja na Kiwanda kidogo cha Kutengeneza Viatu cha watu wenye ulemavu, usafiri Wa Bajaji 36, upandaji Wa miti 2226 Mwenge uhifadhi Wa chanzo cha mto  Mzinga,  Ujenzi Wa Daraja ( Box culvert lenye midomo mitatu ) mtaa wa  Mashine ya Maji, Miradi ya ushonaji kwa Vijana, Usafiri Wa Bajaji 6 , Usafiri Wa Piki Piki 12, Vyombo vya Muziki. Ujenzi vyumba 4 vya Madarasa na matundu 40 ya vyoo Shule ya Martine Lumbanga, Ujenzi miundonbinu Usambazaji Wa Maji, Ujenzi Zahanati ya Charambe, Klabu ya Takukuru na kudhibi dawa za kulevya. 

Aidha amesema kuwa  mwenge wa Uhuru mwaka umebeba kauli mbiu isemayo  Maji ni Haki ya Kila mtu ,tutunze vyanzo vyake na Tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa"

Amesema kuwa pamoja na kauli mbiu hiyo mwenge wa uhuru umebeba ujumbe wa kudumu VVu /UKIMWI chini ya kauli mbiu isemayo pima jitambue ishi,nipo tayari kutokomeza Malaria wewe je? tujenge maisha yetu ,jamii yetu na utu wetu bila dawa za kulevya na ujumbe mwingine uwekezaji katika miundombinu ya maji na utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa maendeleo ya Taifa letu.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.