Header Ads

Kaimu Meya Ilala akabidhi Mabati 100 kusaidia kuboresha madarasa katika Shule za Manispaa Ilala




KAIMU Meya Ilala na Diwani Wa Kata ya Vingunguti, Mh : Omary Kumbilamoto, amekabidhi jumla ya Mabati 100 leo  Julai 30/2019 kwa Mkurugenzi Wa Manispaa ya Ilala .

 Akizungumza na Waandishi Wa Habari leo  Ofisi ndogo za Manispaa zilizopo Kamata ,amesema lengo la  Mabati hayo ni Kuona kwamba Shule zilizo na uchakavu Wa Mabati ziweze kufanyiwa ukarabati .

Amesema kuwa katika Ziara yao ya Jana Julai ya Kamati ya fedha amegundua kuwepo na uchakavu na Mabati kutoboka katika baadhi ya Shule za Msingu na Sekondari.

 Aidha amesema kuwa Mabati hayo yamepatika baada ya mdau kujitokeza kuaaidia kufuatia kuridhishwa na kazi anazozifanya Mh Rais Dkt John Magufuli hususani katika mpango Wa Elimu bure.

 " Tumekabidhi Mabati haya kwa mkurugenzi wetu lakini lengo ni Kuona Shule zetu   zinafanyiwa  ukarabati ili Wanafunzi wasome katika Mazingira mazuri kwani baadhi ya Shule Mabati yamechoka" Amesema Kumbilamoto.

Kwa upande Wa mdau aliyesaidia kujitolea Mabati, Ndugu Kika Edga, amempongeza Mh Rais Dkt John Magufuli kwa kampeni yake  ya Elimu bure. Amesema kilichomsukuna kujitolea Mabati hayo ni kasi ya Rais Dkt John Magufuli ya Elimu bure ambapo kwa sasa Mtoto amekuwa akisoma tofauti na kipindi cha nyuma.

Pia amempongeza Mkuu Wa Wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema na uingozi wake Wa Manispaa kwa kazi kubwa ya kusimamia miradi na Elimu ambapo amefurahishwa na utendaji Wa Kaimu Meya Kumbilamoto huku akizidi kumuahidi kumpa ushirikiano.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.