RC MAKONDA AZINDUA KAMPENI YA USAFI MKOA WA DAR, AGIZA KILA TAASISI ZA SERIKALI MKOA WA DAR KUWEKA WATU WA USAFI MAENEO YAO YA KAZI.
MKUU Wa Mkoa Wa Dar Es Salaam, Mh Paul Makonda amefungua Kampeni ya Mazingira Mkoa wa Dar Es Salaam kwa ajili ya kuweka Jiji safi.
Akizungumza na Waandishi Wa Habari Leo Julai 29/2019 katika uzinduzi huo uliofanyika Uwanja Wa Ndege Terminal 1 ,amesema lengo kubwa ni kuweka Jiji Safi huku akizitaka Taasisi zote za Serikali kuhakikisha kwamba zinakuwa na watu wao Wa usafi katika maeneo yao ya kazi.
Aidha amesema pamoja na kuweka Jiji safi pia ni moja ya maandalizi ya kuwaonesha wageni Wa SADC kwamba Tanzania ipo salama katika usafi hususani Jiji la Dar Es salaam ambapo mkutano huo Wa Marais 16 unakwenda kufanyika.
Amesema kuwa Mkoa Wa Dar Es Salaam unachangamoto ya usafi hivyo ni vyema wakajenga utamaduni Wa kufanya usafi Mara kwa Mara.
Katika hatua nyingine amewataka Vijana wote wanaoingia bara barani kutumia Kanuni za Mazingira katika kuweka Jiji safi.
Vile vile amezihatarisha kampuni za uzoaji taka kwamba zitapoteza tenda zao endapo watakuwa wakichota mchanga na kuweka kati kati ya bara bara.
" Nataka kuwaambia tu kwamba nimemsikia Mratibu Wa Kampeni ya usafi ambaye ni Mkuu Wa Wilaya ya Kigamboni Mh Sara Msafiri ,akisema wapo vijana waliotengwa kufanya usafi hapa, niseme tu hilo jambo nakipinga nataka kila Taasisi ya Serikali katika mkoa wangu iwe na watu Wa usafi badala ya kutegemea watu Wangu wa Mkoani" Amesema RC Makonda.
Amesema ugeni wa SADC ni heshima kwa Rais Dkt John Magufuli na Mkoa wa Dar Es Salaam kwa ujumla hivyo lazima Jiji liwe safi wakati wa kuwapikea wageni pia usafi huo uwe endelevu.
Pia amesema ifikapo Agosti 5 Jiji la Dar Es salaam liwe safi kwa ajili ya mapokezi ya wageni.
Pia amewataka Maafisa Mazingira kuhakikisha miti yote inayopandwa inaota kwani Serikali imekuwa ikitenga bajeti kubwa na pesa hizo hazioneshi matunda na Mazingira chanya kama inavyokusudiwa.
Vile vile amezihatarisha kampuni za uzoaji taka kwamba zitapoteza tenda zao endapo watakuwa wakichota mchanga na kuweka kati kati ya bara bara.
Aidha amewapongeza wamiliki wa vyombo vya Usafiri hususani Dala dala kwa mwitiko wao wa kuhakikisha kwamba ndani ya gari kunakuwa na vyombo vya kuhifadhia taka taka ( Dastibini).
Pia amewataka Vijana wa usafishaji kuhakikisha kwamba Dereva wa gari akitupa taka taka hovyo apigishwe deki kwa kupewa kipande cha bara bara badala ya kuwapiga faini za pesa.
Pia amewataka watendaji wa mitaa husika kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi lasivyo watapoteza ajira zao.
Katika hatua nyingine amewataka Wananchi na Tanzania kwa ujumla wajitokeze kwa wingi katika uzinduzi wa Uwanja mpya wa ndege wa Kisasa wa Mwalimu Nyerere Terminal 3 wenye uwezo wa kubeba Abiria Milioni 6 utakaotarajiwa kuzinduliwa na Rais Dkt John Magufuli Agosti 4/2019 asubuhi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na Mratibu wa Kampeni ya usafi Mkoa wa Dar ,Mh Sara Msafiri, amesema wamejipanga kuhakikisha Jiji la Dar linakuwa safi kwa kila maeneo hususani katika Wilaya zote 5 .
Amesema kuwa zoezi hilo la usafi linahusisha jumla ya Vijana 454, ambapo kati yao Vijana 300 Mgambo Jeshi la akiba, Vijana 130 JKT, na Wakufunzi 24 kutoka kila idara .
Pia amesema katika zoezi hilo limewahusisha Maafisa Mazingira kutoka katika kila Manispaa zote Dar, Maafisa wa Afya wa Kata zote , pamoja na wakandarasi na vikundi vya usafishaji.
Amesema jumla ya Magari 130 yatatolewa na wadau na Magari 30 yatatolewa kwa ajilu ya kumwagilia bara bara .
Post a Comment