DC Mjema ataka miradi ya Kimkakati ikamilike kwa wakati.
MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, ameitaka miradi ya kimkakati ikamilike kwa haraka ili iweze kutoa huduma kwa Wananchi.
Hayo ameyasema leo Septemba 24/2019 wakati Wa ziara yake ya kukagua miradi iliyoko katika Wilaya yake.
Akizungumza na waandishi Wa Habari, DC Mjema, amesema ifikapo mwakani miradi yote iwe imekabidhiwa kwani fedha ishatengwa kwahiyo hakuna haja ya kuchelesha miradi.
Aidha katika hatua nyingine DC Mjema ametembelea mradi Wa Soko la kisasa la Kisutu na kuridhishwa na kasi ya mradi huo lakini aliwaomba wakimbizane na muda.
Pia ametembelea mradi Wa Mabweni ya Kike Shule ya Sekondari Jangwani ambapo mradi huo unagharimu Milioni 162 wenye jumla ya kubeba Wanafunzi 160 ambapo kila bweni litachukua wanafunzi 80.
Pia amepata nafasi ya kutembelea Machinjio ya kisasa ya Vingunguti huku akiahidi kero zilizopo kuzitatua ambapo mradi huo unaendelea lakini kero zilizoibuka zilitokea machinjio ya zamani na kupokea malalamiko ya wafanya Biashara Wa Utumbo Wa kitabu pamoja na damu.
" Nimeanza leo ziara nimeona miradi yote lakini nataka kasi iongezwe ili ifikapo mwakani tuikabidhi kwahiyo endeleeni na kazi panapo kwama mtufahamishe tuone tunakwamuanaje" Amesema Mjema.
Hata hivyo ametembelea Shule ya Pugu Sekondari na kutaka wale waliovamia maeneo ya shule Sheria itachukuliwa huku akitaka mradi Wa Biogas ufanyiwe kazi baada ya kusimama tangia 2014.
Pia katika hatua nyingine amemtaka Injinia aongeze mafundi katika mradi Wa Hospitali ya Kivule ili kasi ya ujenzi iongezeke.
Post a Comment