*RC MAKONDA KUWACHUKULIA HATUA WANAOWADHALILISHA WAHUDUMU WA BAR NA WAFANYAKAZI WA NYUMBANI*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* amepanga kukutana na makundi ya watu mbalimbali ikiwemo *wahudumu wa Bar, Hotel, wafanyakazi wa Saloon na wafanyakazi wa nyumbani* kwa lengo la kusikiliza *kero na malalamiko* yao baada ya kubaini wengi wao wamekuwa wakifanyiwa *vitendo vya udhalilishaji* na unyanyasaji ikiwemo *kutolewa lugha za matusi* kutoka kwa baadhi ya *wanaume wasiojiheshimu.*
*RC Makonda* amesema kuwa katika *mkutano* wake na makundi hayo atataka kufahamu masuala ya *mishahara, ajira,changamoto wanazopitia na suala zima la usalama wanaporudi majumbani usiku wa manane* ambpo ameeleza kuwa anachokitaka ni kuona *kila mtu anaheshimu kazi ya mwenzake.*
Hayo yote yamejiri leo wakati wa maadhimisho ya *Siku ya wanawake* yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City.
Post a Comment