Header Ads

DAS ILALA ATAKA JUMUIYA YA WATUMIAJI MAJI IWE NA 60% YA WANAWAKE.



KATIBU Tawala Wilaya ya Ilala , Sheila Edward Lukuba ,ameweka Jiwe la Msingi Ujenzi Wa Tanki la  Maji Majohe. Akizungumza na Waandishi Wa habari, amesema katika Kuona mradi huo unawanufaisha watu wengi lakini Jumuiya ya Watuniaji Maji wawe Wanawake kwa Asilimia 60%.

amesema kuwa mradi huo wa maji umejengwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA na utawasaidia wananchi wote wanaoishi mtaa wa Kichangani Mahoje.
Pia amesema kuwa, taarifa za mapato na matumizi kikao kifanyike kila mwezi na fedha hizo zitumike kutunza miundombinu ya Maji. 

Hata hivyo amesema,Ofisi ya Mkurugenzi inatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ibara No 55 ya kumtua ndoo mama kichwani ifikapo 2020 tunawapongeza sana

Amesema kuwa, gharama za mradi huo ni takribani milioni 230 na unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa nne na lengo kuu ni kupunguza kero ya maji kwa wananchi.

Upendo amesema, serikali kwa kushirikiana na mamlaka za maji wanaendelea kushirikiana kwa pamoja kupeleka maji kwenye maeneo ambayo hayakuwa na mtandao wa maji na kufikia lengo la asilimia 95 mwaka 2020.

“Kuna mradi mwingine wa maji unaosimamiwa na DAWASA wa Ujenzi wa tanki la Kisarawe ambapk kufikia mwishoni mwa mwaka huu wananchi wote wa Majohe na Gongo la Mboto kaa ujumla watapata majisafi na salama,”amesema Upendo.


Diwani wa Kata ya Kichangani Mwanevyale Waziri ameishukuru ofisi ya Mkurugenzi kwa kufanikisha kuja kwa mradi huo kwani wana muda mrefu wananchi wa eneo hilo hawajapta majisafi na salama.

Mradi huo wa maji wa Mtaa wa Kichangani utakapomalizika kutajengwa vizima saba vya kuchotea maji kwa ajili ya kuwarahishia wananchi wa maeneo hayo.

DAWASA wanaendelea kuadhimisha wiki ya maji iliyoanza Machi 16 na itamalizika Machi 22 ikiwa na kauli mbiu ya Hakuna atakayeachwa.
 Katibu Tawala DAS Ilala Sheila Edward akiwa sambamba na Diwani wa Mtaa Kichangani Mwanevyale Waziri wakiweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Ilala Upendo Lugongo akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko akizungumza na wananchi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.