Wapotoshaji zoezi la vitambulisho vya wajasiriamali kukiona cha mtema kuni - DC MJEMA
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mh: Sophia Mjema, amesema hayupo tayari kuwaacha wale wanaopotosha zoezi zuri la Mh Rais John Magufuli la kuwapa Vitambulisho Wajasiriamali. Hayo ameyasema leo kwenye Ofisini yake wakati wa mahojiano na Tumaoni Tv.
DC Mjema, amesema mpaka sasa wanawashikiria watu wawili ambao walikuwa wakisambaza taarifa za uongo ambazo zilikuwa zikifanya zoezi hilo kuwa gumu.
Amesema watu hao walikuwa wakisambaza taarifa za kusema utoaji wa vitambulisho ni moja ya mbinu za kodi ya kichwa kitu ambacho hakina ukweli Wowote na ni upotoshaji mkubwa.
Amesema lengo la Mh Rais ni kuona wamachinga wanatambuliwa na kuongeza uchumi kutoka kipato kidogo kufikia kipato cha kati.
Amesema watu wasiogope zoezi hilo kwani vitambulisho hivyo havina TIN namba na wale watakaopata hivyo vitambulisho wasitoe ushuru wowote zaidi ya pesa waliyolipia kupata hivyo vitambulisho.
" Hili ni zoezi huru, zoezi zuri ambapo Mh Rais wetu ameonesha upendo kwetu na kutujari sasa hivi wachinga wanatambuliwa na wanafanya Biashara zao kwa uhuru zaidi tofauti na mwanzo hivyo chukueni vitambulisho na wale wapotoshaji tunakwenda kuwashughurikia " Amesema DC Mjema.
Pia amesema wale wanaotaka vitambulisho waende katika kata zao watapewa.
Pia amesema changamoto ya vitambulisho feki katika Wilaya yake hakuna na kama wapo watafikishwa kwenye vyombo vya Sheria huku akisema hakuna vitambulisho vya elfu 5000 wala elfu 7000 na watu binafsi vilivyopo ni vya Rais peke yake.
Amesema Ilala, ipo huru na wale ambao hawajamaliza katika Wilaya zao ruksa kuvipeleka kwao kwani lengo ni Kuona vitambulisho vinaisha katika mkoa wa Dar Es Salaam.
Amesema watu wasiogope kulipa kodi kwani ndiyo inayofanya nchi yetu kuwa na miundombinu mizuri, pamoja na huduma za Afya na hivi karibuni Rais katoa misaada nchi tatu zilizokumbwa na mafuriko hiyo yote ni kutokana na kodi za ndani.
DC makini kabisa..Mungu amlinde kwa maslah ya Taifa
ReplyDelete