DAS Ilala atekeleza agizo la DC kukomesha vitendo vya unyanyasaji kazini
KATIBU Tawala Wilaya ya Ilala, Sheila Lukuba, ameanza kutekeleza agizo la Mkuu Wa Wilaya Ilala, Mh Sophia Mjema, la kuweka Sanduku la maoni katika kuwafanya Watumishi Serikalini na Sekta binafsi kuwa huru kutoa Mani dhidi ya vitendo viovu.
Hayo ameyasema leo Mara baada ya kutambulisha rasmi Sanduku la maoni Ofisini kwake Ilala.
Amesema Sanduku hilo la maoni ni agizo la Mkuu Wa Wilaya Ilala, Mh Sophia Mjema, alilolitoa kwenye hafla ya kusherekea Siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na Chama cha Wafanyakazi Serikali za Mitaa Mkoa Wa Dar Es Salaam kwenye Hoteli ya Deluxe iliyopo Sinza Kijiweni.
Aidha amesema kuwa, dhumuni la Sanduku hilo ni kuwafanya Watumishi wa kike kutoa Taarifa ya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia .
Amesema Sanduku hilo la maoni litawafanya Wanawake Watumishi kuwa huru na na wale wote watakaobainika kuwa na tabia hiyo watachukuliwa hatua Kali za kisheria .
Amesema kitendo cha unyanyasaji Wa kijinsia ni kinyume na Sharia ya ajira na mahusiano kazi Namba 6 ya mwaka 2004.
" Tumeanza kutekeleza agizo hili tulilopewa na Mkuu wetu na sasa tunalifunga hapa Ofisini kwa kuzingatia eneo litakalofikika kwa watu wote na ndugu zetu wenye ulemavu wapate fursa ya kutoa maoni yao, tunamshukuru Mkuu wetu Mama Sophia Mjema kwa kuwa karibu na Wanawake hii inaonesha ni kwa jinsi gani anatekeleza vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuelekea Uchumi Wa kati na Tanzania ya Viwanda kwa kuwawezesha Wanawake , Wakina mama, Vijana na Walemavu" Amesema Das Sheila.
Ikumbukwe kwamba agizo hilo lilitolewa kwa Wilaya zote kwa makatibu Wa Wilaya kufanikisha zoezi hilo ambapo Wilaya ya Ilala imeanza mapema kumkomboa Mwanamke. Miongoni Mwa Vitendo wanavyokutana navyo Watumishi Wa kike ni pamoja na Rushwa ya ngono , udharirishaji Wa kijinsia na kudharaurika.
Post a Comment