Kaimu Meya Ilala ageuka mbogo juu ya pesa za Mfuko wa Jimbo zilizoombwa na kamati za Shule na kuingizwa akaunti za kata.
KAIMU Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto, ametoa agizo Kali la kutaka pesa zote zilizoombwa na Kamati za Shule na kuingizwa katika akaunti za Kata zirudishwe kwa wenyewe ili miradi iliyokusudiwa itelelezwe.
Hayo ameyasema leo Mara baada ya kufanya ziara fupi ya kushtukiza katika shule za Msingi Liwiti na Kimanga.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Kumbilamoto , amesema kitendo cha Kata kuingiziwa pesa za mfuko wa Jimbo ile hali hawajaziomba wao kimefanya miradi iliyokusudiwa ikiwamo ukarabati na Ujenzi wa madarasa kuchelewa.
Amesema kuwa watendaji wengi wamekuwa chanzo cha kukwamisha miradi ambapo matokeo yake Viongozi wa ngazi za juu wanatupiwa lawama za kuonekana kukwamisha utekelezaji wa Ujenzi.
Amesema kuhusu kesi ya Shule ya Msingi Liwiti kuna uzembe uliofanywa ambao una lengo la kitaka kumchafua Mbunge wa Jumbo la Segerea.
Katika Kuona mgogoro huo unafikia mwisho, amemtaka Mtendaji wa Liwiti kuhakikisha anarudisha Ujenzi huo kwa Kamati ya shule na Idara ya uchumi wahakikishe pesa hizo zinarudishwa haraka ili Ujenzi uendelee.
" Ikumbukwe kwamba hizo pesa ziliombwa na Kamati za shule kwahiyo kamati ya Jimbo ilitoa baraka zote iweje mpaka sasa Ujenzi haufanyiki? Tunataka Kuona matokeo tunatakiwa kumsaidia Rais wetu kuhakikisha miradi yote iliyoyengewa fedha inakamilika sasa mpaka jumatatu mwalimu Mkuu kutana na Injinia ukabidhiwe mchoro na BOQ Ujenzi uanze haraka sana" Amesema Kumbilamoto.
Licha ya shule ya Liwiti nako kunako shule ya Msingi Kimanga hali zikafanana ambapo pesa ilitolewa na mfuko wa Jimbo kutengeneza madarasa 2 zimringizwa kata lakini agizo lake kufikia jumatano Aprili 3 , 2019 Ujenzi uwe umeanza na kama hawajaanza pesa zote zirudishwe Kamati ya shule.
Ametoa agizo kwa Idara ya uchumi kupeleka pesa kwa waliohitaji na kumtaka Afisa Utumishi kumtafutia uhamisho Mtendaji Liwiti.
Post a Comment