DC Mjema akabidhi mradi wa Ujenzi Hospitali ya Wilaya Ilala kwa JKT
Mkuu Wa Wilaya ya Ilala, amefunga mkataba wa Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilala kutoka kampuni ya Ujenzi ya Scoll na kuwakabidhi JKT baada ya kushindwa kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati. .
Akizungumza na Waandishi wa habari leo kwenye mradi huo, DC Mjema amesema Ujenzi huo umekuwa ukigubikwa na siasa za hapa na pale jambo ambalo limesababisha kutokukamilika kwa wakati..
Amesema kuwa , Ujenzi huo ulitakiwa kumalizika mapema kwani tangia wawakabidhi mwaka 2016 hadi Leo hakuna kinachoendekea.
Amesema kwa sasa Serikali ya awamu ya tano inataka miradi yote iliyoingiziwa fedha iwe imeshaanza na kuonesha matumaini jambo ambalo kwa Ujenzi wa Hospitali hiyo haukufanyika zaidi ya hadisi tuu.
Katika Kuona Ujenzi huo unakamilika kwa wakati DC Mjema ameukabidhi mradi huo wa vyumba vya kulazia wagonjwa na kulipia na wale wenye bima kwa Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) kutoka kwa Wakala wa Majengo Tanzania.
Amesema ifikapo Tarehe 1 Aprili 2019, mwandisi mshauri awe amekabidhi michoro yote kwa Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT).
" Nimeamua kuwa mkali sana huu Ujenzi unatufanya kuonekana hatufanyi kazi sasa nimeamua kufanya maamuzi magumu kuwakabidhi mradi huu JKT nataka haraka sana michoro ikabidhiwe na kazi ianze Mara moja" Amesema DC Mjema.
Naye Mwandisi wa Manispaa ya Ilala, Justine Magoda, amefurahishwa na uamuzi wa DC Mjema na kusema kwamba uamuzi huo una manufaa makubwa ya kuhakikisha mradi huo unakamilika na wananchi wanapata huduma.
Pia amesema changamoto kubwa iliyopelekea kucheleweshwa kwa Ujenzi huo ni kukosekana kwa mwandisi mshauri katika michoro.
Post a Comment