Naibu Meya ahidi makubwa Vijana Boda Boda Vingunguti katika upatikanaji Wa Mikopo.
NAIBU Meya Wa Manispaa ya Ilala na Diwani Kata ya Vingunguti, Mh Omary Kumbilamoto, Leo amekutana na Dereva Wa Boda Boda Vingunguti kutoka Maskani ya Scania katika kutoa elimu ya Mikopo .
Katika Mkutano huo, ameeambatana na Afisa Vijana Manispaa ya Ilala pamoja na Mlezi katika maadili ya watoto pamoja na utoaji elimu ya ujasiriamali Bi Eva Kapinga.
Akizungumza na Waandishi Wa Habari, Kumbilamoto amesema kuwa semina hiyo ya Mikopo ameifanya ili kuwajengea Vijana wake uwezo Wa kujiamini katika mikipo hiyo ya Manispaa.
Amesema Vijana wengi haswa Manispaa ya Ilala Pembezoni zoezi hilo limekuwa likisuasua kwa ajili ya kukosa ujasiri Wa kukopa.
Amesema Manispaa yake imetenga Milioni 153 na mpaka sasa ni vikundi 44 vimeshapatiwa fedha ambapo kati ya vikundi 7 ni Vijana na vikundi 2 ni upande Wa Walemavu.
Amewataka Vijana wachangamkie fursa kwani matajiri wote Duniani ni wafanya Biashara
Amesema nia ya Manispaa kuweka kipengele cha nyumba kama dhamana siyo kwa ajili ya kuchukua nyumba Zao Bali ni kutaka kuonesha watu juu ya matumizi mazuri na nidhamu ya fedha.
" Hii ni fursa adhimu sana Leo nipo nitumieni mta kaa miaka 20 hamtampata Naibu Meya katika kata hii, Walemavu washapata cheti , wewe mwenye viungo kamili unaogopa nini? Lengo letu tunakukopesha ili uachane na Biashara ya utumwa na umiliki chombo chako mwenyewe" Amesema Kumbilamoto.
Naye Afisa Vijana Manispaa Bi Sapiencia Masaga, amesema Mikopo hiyo hutolewa kwa wale wenye Biashara ili kuongeza kipato .
Amesema Mikopo hiyo huzingatia umri ambapo kwa upande Wa Wanawake kuanzia miaka 18-60 na kwa wanaume kuanzia miaka 18-35.
Amesema kitu kikubwa katika Mikopo hiyo ni uaminifu na kuwa mkweli na kadri unavyolipa deni lako kwa haraka na wakati unapata nafasi ya kukopa zaidi.
Post a Comment