Header Ads

DC Mjema aungana na TALGWU kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.















MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, leo ameungana na TALGWU kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Hafla hiyo fupi imefanyika katika Hoteli ya Deluxy iliyopo Wilaya ya Kinondoni Sinza Kijiweni.

Akizungumza na Waandishi Wa habari, DC Mjema , amewapongeza TALGWU kwa maandalizi mazuri ya Kuwakumbuka Wanawake Duniani.

Amesema kuwa licha ya Wakina Mama kukabiliwa na changamoto mbali mbali lakini wamekuwa wakichangia kwa asilimia 80% ya Maendeleo hususani Vijijini katika Sekta ya Kilimo.

 Aidha amewataka wakina mama kujiamini kwani wao ndio Msingi Wa Maendeleo katika familia.

" Tunaposherekea siku kama ya Leo tunapaswa kujiamini kwani sisi tunamchango mkubwa sana katika Maendeleo vijijini, sisi ndio wakulima wakubwa hivyo lazima Mwanamke atembee kifua mbele " Amesema DC Mjema.

Pia amewataka wakina mama kushughulika na mfumo Wa umilikiji Wa Ardhi ili kuepusha migogoro katika familia pale inapotokea familia kutengana au baba kufariki . .


Amesema Ofisini kwake amekuwa akitatua kero mbali mbali zinazohusu migogoro ya Ardhi hivyo kama wakina baba hawashughuliki navyo wao wanatakiwa kupata hati ya Ardhi .

"Migogoro mingi husababishwa na Wanawake kukosa hati hivyo hupelekea  kutapeliwa na watu wengine na kujikuta ukiishi maisha magumu ukiwa hujui la  kufanya " Ameongeza DC Mjema.

Kuhusu asilimia 50% kwa 50%, amesema  kila Mwanamke amuheshimu mume wake kwani ndani ya nyumba hakuna Nguvu sawa kwani mwenye Nguvu kubwa ni mwanaume hivyo Wanawake wanatakiwa kuwakamata waume zao ili wasichepuke lakini katika shughuli za kiuchumi huko ndipo tunatakiwa kuwa sawa na wanaume.

 " Tumeomba kazi tuzifanye kazi, kama upo kikazi usiku piga simu mwambie mume wangu nipo kwenye daraja unasikia vyuma vinalia? Hapo utakuwa umemridhisha huku ukiendelea kupiga kazi kwa Maendeleo ya Taifa" Amesema DC Mjema.


 Hata hivyo amepiga vita ya ngono Ofisini huku akiwataka wenye tabia hizo waache Mara moja kwani ni kinyume na sheria na inapunguza utendaji Wa kazi.

Amewataka Wanawake waanzishe Sanduku la  maoni kwa ajili ya kuelezea kero Zao katika ofisi zao.

Amewaomba wakuu  wa Wilaya kutengeneza timu itakayo kuwa ikikutana na wananchi wao kwa ajili ya kusikilizwa kero zao ikiwezekana kuongeza Timu ya mawakili wa  nje kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama kupata haki zao Mahakamani.

Naye Bi Janeth Suda, Mwenyekiti Wa Kamati ya  ushauri Wanawake TSLGWU Mkoa Wa Dar Es Salaam, amempongeza DC Mjema kuhudhuria katika hafla hiyo fupi ya siku ya Wan awake Duniani.

 Pia amewataka wakina mama kuacha kukwepa majukumu yao na kujiona wanyonge kwani wao wanategemewa katika Taifa hili kuelekea uchumi Wa kati.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.