DIWANI MBURAHATI KUJENGA UWANJA WA KISASA WA MPIRA WA MIGUU
OFISI YA MHESHIMIWA DIWANI KATA YA MBURAHATI.
Uwanja huu pichani ni Uwanja wa Mpira wa Miguu Santos uliopo katika Mtaa wa Barafu. Uwanja huu sasa unaenda kuwa Uwanja wa kisasa kwa kupandwa nyasi safi kabisa.
Utengenezaji wa Uwanja huo unafanywa chini ya Shirika la BORDA ambao ndio waliofanikisha kuanza kwa Ujenzi wa Uwanja huu.
Kipekee kabisa mimi Mhe. Diwani wa Kata ya Mburahati Mhe. YUSUPH OMARY YENGA nililiomba hili kupitia kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo alipofanya ziara ya kukagua Mradi wa kuchakata maji taka ambao Mradi huo upo jirani na Uwanja huu wa Mpira. Ziara hyo ilikuwa July 21, 2018. Niishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI hakika ameteua Watumishi ambao wanawafikia Wananchi walipo.
Katika kuhakikisha kuwa nawaletea Maendeleo wana Mburahati nililiomba suala hili kwa mapenzi ya dhati kabisa kwa Wananchi wangu wa Mburahati.
Kukamilika kwa Uwanja huu itakuwa fursa nzuri sana kwa Vijana wetu kupata mahala salama na rafiki kucheza. Pia itapelekea watu wengi kuja kuona Mburahati kuna nini na kufungua fursa kwa Vijana wetu kuonekana na kupata Ajira kupitia mpira.
Pia itafungua wigo na fursa za Kibiashara kwa watu wengi sababu kukamilika kwa Uwanja huu kutapelekea watu wengi kuja kuangalia michezo.
Niwaombe Wakazi na Wananchi wote wa Kata ya Mburahati kuwa wavumilivu pale ambapo Mradi huu utaanza rasmi kwa sababu ni kwaajili yetu.
Nilihaidi kuwatumikia na naendelea kuwatumikia na ntazidi kuwatumikia zaidi.
"Mburahati mpya itajengwa kupitia mm na wewe "
Post a Comment