Header Ads

Diwani Kata ya Kipawa awataka Wazazi kutotegemea Miujiza kufaulu kwa Watoto wao





















DIWANI wa Kata ya Kipawa, Kennedy Simion, amesema Wazazi wasitegemee miujiza kuona Watoto wao wanafaulu. Hayo ameyasema Leo wakati akimuwakilusha Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, kwenye Mahafali ya Shule ya Sekondari Kinyerezi.

Diwani huyo, amesema Wazazi wanatakiwa wawe na mipango na mikakati ya kumsaidia Mtoto wake aweze kufanya vizuri.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, amesema Baadhi ya Wazazi wanachangia kufeli kwa watoto wao kutokana na katabia walicho jijengea cha kuwapeleka watoto Shuleni na kuwaaga bila ya kufuatilia maendeleo yao.

" Hii sio tabia nzuri kwa Wazazi, mnatakiwa mtengeneze daraja zuri  la  kuwavusha watoto wenu na daraja hilo ni kushirikiana na waalimu na kuhudhuria vikao vya shule, lakini kama tutazidi kuona swala hili ni la  waalimu pekee bado tutakuwa tunatengeneza Zero za watoto wetu na kumkatisha ndoto yake" Amesema Diwani Kennedy. Amesema ili Wanafunzi wafaulu wanahitaji mikakati, kujiandaa , kujiamini pamoja na kuwa na ndoto  ya kutaka kuwa mtu  Fulani.

Amesema wapo baadhi ya Wazazi wao kila siku wanapiga stori  na watoto wao kuhusu mpira wa Miguu wakati muda huo angeutumia kufuatilia maendeleo ya Mtoto wake . Naye Diwani wa Kata ya Pugu, Bonaventure  Mfuru, Amesema ili Wanafunzi wafaulu wanahitaji kujikita sana katika kujisomea.

" Huu ni mitihani kwa Wazazi lakini kama unampa utaratibu mwanao na unamfuatilia kuhakikisha anajisomea atafaulu mitihani yake pamoja na kuwa na maendeleo mazuri katika masomo yake" Amesema Mfuru.

  Pia Amesema mwakani wanatarajia kuwa na Shule ya Msingi Kinyamwezi kwa gharama ya Shilingi Milioni 20.

 Katika hatua nyingine, Mkuu wa Shule ya  Kinyamwezi,Bi Sifa Mwaruka, amempongeza Diwani huyo kwa kuacha kazi zake na kujumuika katika Mahafali hayo. Pia amewataka Wanafunzi wasome kwa bidii kwani kila kitu kinawezekana .

 Amesema shule yao ilianza changa sana lakini Leo imepanuka licha ya kukabiliwa na Changamoto nyingi. Amesema  Wazazi walijitahidi kushirikiana na waalimu wakapata madarasa mawili .

Amesema kuwa wingi wa Wanafunzi unawasababishia kushindwa kufikia katika malengo ya ufundishaji kutokana na uhaba wa Madarasa.

 Aidha amesema taaluma ina kwamishwa na mambo Makuu mawili la kwanza ni utoro na lingine ni miundombinu kitu kinachopelekea Wanafunzi kuchelewa Shule na kupelekea wengine kutohudhuria darasani kwa kuhofia adhabu.

 Amewapongeza Wadau pamoja na Wananchi wenye  mapenzi mama na Shule ya Sekondari Kinyerezi.

" Tunakushukuru mgeni rasmi, kama ulivyosikia kwenye risala , changamoto za madarasa, Maabara , waalimu, vitendea kazi pamoja na miundombinu tunakuomba haya matatizo mtu  saidie " Amesema Madam Mwaruka.

 Hata hivyo amezungumzia ufinyu wa Uwanja wa mchezo hadi kupelekea wachezaji kuwa pungu kwa kila timu kuwa na wachezaji 6 .

Akijibu kero hiyo , Diwani Kennedy amesema wapo katika mchakato wa kuleta   Greda  kwa ajili ya upanuzi wa kiwanja hicho.

Pia katika Mahafali hayo tulishuhudia vipaji mbali mbali vya ulimwende pamoja na maigizo yenye ujumbe kwa Wahitimu yaliyoandaliwa na Wanafunzi hao. Licha ya maigizo zilitolewa zawadi mbali mbali ikiwamo za washindi wa Kombe la Mwaruka, nidhamu, Uongozi pamoja n usafi bora .

 katika Mashindano hayo ya Mwaruka Cup mshindi alijinyakuria Jogoo mmoja na washindi walikuwa Form3.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.