RC MAKONDA AUNDA KAMATI YA KUWAADABISHA MASHOGA NA WANAOFANYA BIASHARA YA NGONO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* leo ameunda *kamati ya watu 17* watakaofanya *operesheni kabambe* ya kuwafundisha adabu watu wanaofanya *ushoga, nyumba zinazotumika kurekodi video za Ngono, wanaojiuza na matapeli* wa njia ya mitandao.
*RC Makonda* amesema kamati hiyo inajumuisha maafisa wa *Polis, TCRA, Wanasheria, Bodi ya Filamu, Madaktari* na Wataalamu wa *ushauri na Saha* ambapo kamati hiyo itaanza *zoezi la kamatakamata* jumatatu.
Operesheni hiyo imepokelewa kwa *mikono miwili* na *mamilioni* ya wananchi ambao wamekuwa *wakichukizwa* na mmomonyoko wa maadili ambapo *RC Makonda* hadi sasa amepokea *SMS zaidi ya 18,000* za watu wanaopongeza na kutaja majina ya watu wanaofanya *matendo maovu* ikiwemo *ushoga na biashara ya ngono.*
Aidha *RC Makonda* amesema hadi sasa amepokea *majina zaidi ya 200* ya mashoga waliotajwa wakiwemo kina *James Delicious, Dida Mtamu,Abas,Aunt Miliki* na kundi la *Pachupachu.*
Pamoja na hayo *RC Makonda* amesema oparesheni hiyo pia itahusisha *sehemu za Masaji* ambazo baaadhi yake zimekuwa zikijihusisha na *biashara ya ngono*.
Hata hivyo *RC Makonda* amesema kuwa hata *wanaume watakaotajwa* kuwa na *mahusiano ya kimapenzi* (wateja) wa *Mashoga* watakamatwa na kuchukuliwa hatua Kali za kisheria kwa mujibu wa Sheria.
Sanjari na hayo *RC Makonda* ametoa *angalizo kwa watu wenye picha na video za ngono kwenye simu* zao kuwa *operesheni hii haitowaacha salama.*
*WAZAZI TUSHIRIKIANE KUPINGA USHOGA NA BIASHARA YA NGONO.*
Post a Comment