Header Ads

Jumla ya Washiriki 1500 kujitokeza kushiriki zoezi la Medani la Ushirikiano imara wa Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashiriki Mkoani Tanga.





JESHI la  Wananchi hapa nchini, JWTZ , limesema wapo mbioni kuanzia zoezi la  Medani lijulikanalo  kama Ushirikiano imara litakalo Shirikisha nchi 6 wanachama  wa Jumuiya  wa Afrika Mashariki ( EAC),  yatakayo fanyika Jijini Tanga.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkuu wa Tawi la  Operesheni Mafunzo JWTZ, Meja Jenerali, Alfred Kapinga, Leo amesema Zoezi hilo la  Medani  ya  Majeshi yatafanyika katika Wilaya mbili ikiwamo  Wilaya ya Tanga Mjini pamoja na Wilaya ya Muheza.

Amesema Tanzania hii ni fursa ya Pili kupata kuwa mwenyeji wa  Mazoezi makubwa ya Kijeshi ambapo mwaka Jana  walifanya zoezi la  Matumbawe yaliyoshirikisha  nchi zilizopo katika Jumuiya ya SADC.

Aidha  amesema kuwa Katika Zoezi hilo la ushirikiano imara Mkoani Tanga, Wilaya ya Muheza ndiyo iliyopendekezwa kuwa makao makuu hadi pale zoezi hilo litakapomalizika.

Amesema Katika Mazoezi hayo watakayo fanya, yatashirikisha majeshi ya nchi kavu, Anga  pamoja na majini.

Amesema matarajio yao ni kuona kwamba kila Idara na Majeshi yote hapa nchini yatashiriki ili kuweza kutengeneza muungano imara katika kuimarisha ulinzi na Usalama wa Jumuiya hizo.            

Miongoni Mwa Mataifa yatakayoshiriki katika mazoezi hayo ya pamoja na Rwanda, Uganda, Kenya,  Burundi,  na Tanzania Sudani Kusini.

Amewataka Wananchi wa Tanga waongeze Upendo na moyo walio uonesha wazidi kuonesha  tena katika Katika Mazoezi hayo  ya ushirikiano imara  yanayotarajia kutimua  vumbi Novemba 5 hadi 21 mwaka huu.


 " Dunia kwa Sasa imebadilika hata ukiangalia mtazamo wa utendaji kazi umebadilika na hata vita ya mipaka imepungua huku vita ya ugaidi pamoja na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe" Amesema Meja Jenerali  Kapinga.

Kuhusu zoezi hilo  kufanyika Tanga, amesema Mkoa huo Kijiografia upo vizuri  kama Uwanja wa ndege, bandari kwa ajili ya mazoezi ya majini  pia ni mkoa ambao umepakana na nchi jirani watakao jitotokeza katika Mafunzo hayo.  
         
Akijibu swali la  mwandishi wa Habari kuhusu gharama za Mazoezi   hayo, Meja Jenerali Kapinga, amesema  kila nchi itachangia kuanzia gharama hizo pamoja na kuja na huduma zao.

Katika hatua nyingine, licha ya kupata Mazoezi  hayo amesema zipo faida mbali mbali ikiwamo mkoa husika kunufaika na ugeni huo kiuchumi kutokana na kujenga vyumba viwili vya kisasa na ofisi za kisasa katika Shule ya  Sekondari , Machemba iliyopo Wilayani Muheza.

Miongoni Mwa faida nyingine alizozitaja ni pamoja na kujenga uwezo wa Majeshi katika kukabiliana na ulinzi na usalama ikiwamo ugaidi ,uvamizi wa mpaka , uvamizi wa Bahari pamoja na Majanga ya asili, kubadilishana uzoefu wa kiutendaji na kudumisha na kuimarisha mahusiano  ili kuweka uadui mbali tofauti na mkiwa mbali mbali mnakaribisha uadui wa karibu.

Licha ya uwepo wa mazoezi hayo, lakini wanatarajia kufanya shughuli za kijamii zikiwamo mazoezi ya Kijeshi, huduma za kijamii pamoja na kuwahudumia wagonjwa na kuwapima bure.

Amewataka  wakazi wa Tanga wakae mkao wa kula na watanufaika na mazoezi hayo Mara baada ya kumalizika.

Naye Kapteni Nuru amesema hii ni fursa hivyo amewataka Waandishi wa Habari wajitokeze kwa wingi katika kuyatangaza mazoezi hayo yatakayo waletea Sifa Majeshi yote na Tanzania kwa ujumla.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.