MHE MABULA ASHIRIKI CHAKULA NA WANAFUNZI SHULE YA AWALI SOS
Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula ametembelea uwekezaji wa shule ya awali "Serve Our Soul Children home Kindergarten" inayolenga kutoa elimu bora kwa watoto waishio mazingira hatarishi. Mhe. Mabula akiwa shule hapo amepongeza taasis ya SOS kwa uwekezaji mkubwa wenye dhima yakujenga Misingi imara ya elimu bora na kuondoa athari zinazoweza kutokana na mtoto kuwa katika mazingira magumu na hatarishi pamoja na kuwa na taifa lenye wananchi tegemezi. Sanjari na hayo Mhe. Mabula ameshiriki chakula cha mchana pamoja na kula cake na wanafunzi hao.
Naye Kaimu meneja SOS tawi la Mwanza Ndg. Samson amesema SOS imedhamilia kuwekeza katika sekta ya elimu Wilayani Nyamagana, ikiwa ni pamoja na shule ya awali inayotoa elimu kwa kufuata mitaara ya Mentosori, elimu ya msingi kwa kujengea miundombinu yote katika shule ya Msingi na Sekondari Igelegele, pamoja na shule mbali mbali katika kata tano za Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Katika ziara hii Mbunge Jimbo la Nyamagana aliambatana na ujumbe wa taasis ya First Community Organizations ukiongozwa na Mwenyekiti Ahmed Misanga, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Kata, Mtendaji wa serikali Kata na Mtaa pamoja na viongozi wa SOS.
Post a Comment