DAS Ilala apongeza jitihada za Manispaa Kitengo cha Usafishaji na Mazingira katika zoezi la ugawaji Dastibini Kata ya Gerezani.
KATIBU Tawala Wilaya ya Ilala , Sheila Edward, ameupongeza Uongozi wa Manispaa hususani Kitengo cha Usafishaji na Mazingira kwa kutoa Dastibini Kata ya Gerezani na pembezoni Mwa Bara bara ya Kariakoo Msimbazi ikiwa na lengo la kuhakikisha Manispaa ya Ilala na viunga vyake inakuwa Safi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ugaiwaji Dastibini hizo , DAS Sheila , amesema usafi liwe suala la kudumu na endelevu ili kuchangia kustawi kwa Mazingira ndani ya Manispaa hiyo.
Amesema ni wakati Sasa Wananchi wakalichukulia suala hili la usafi kama suala nyeti linalotakiwa kupewa kipaumbele pasipo mtu kutumwa wala kusimamiwa.
Amesema wapo Wananchi wanaokatisha tamaa jitihada za Viongozi kuhusu suala la usafi, hivyo amewaomba watu wote na jamii kwa ujumla kuunga mkono zoezi la usafi kwa mikono miwili.
Hata hivyo , DAS Sheila, amesema kuwa huo ni mwendelezo wa usafi wa Kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mh: John Magufuli wa kutoka Tanzania iwe katika muonekano mpya katika kupiga vita maradhi yatokanayo na ugonjwa wa milipuko shauri ya uchafu.
Amesema kuwa kwa kushirikiana na ofisi mbali mbali na Kitengo vyake ikiwamo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa , Mkuu wa Wilaya na Manispaa watahakikisha zoezi la usafi na Mazingira linasimamiwa kidete lengo ni kuona Mkoa wa Dar es Salam unakuwa msafi.
Pia amewataka Wananchi wahakikishe kwamba Dastibini hizo zinatumika katika kuhifadhia taka taka nyepesi kama vile vipisi vya Sigara , karatasi za Pipi, mifuko mikavu pamoja na Chupa za Maji zisizokuwa na Maji .
" Huu ni mpango wetu wa kuhakikisha Dar na Manispaa ya ilala inakuwa safi, Dastibini hizo tumetumia Pesa kuzinunua Sasa sitarajii kama ntakutumia vibaya kinyume na matumizi yaliyokusudiwa, nataka kuona zinatunzwa vizuri pia kwa wale ambao watakwenda kinyume kutupa taka taka nje ya Dastibini faini zitawahusu" Amesema DAS Sheila.
Amesema kwamba faini zinajieleza na zimewekwa kwa mujibu wa vifungu vidodo vya Sheria elekezi ya Mazingira ambayo faini yake inaanzia Shilingi Elfu Hamsini 50,000/= hadi Milioni hii inatokana na ukubwa wa iana ya uchafu uliofanyika.
Amesema Dastibini hizo zimefungwa pembezoni Mwa bara bara ili kila mwananchi atimize wajibu wa usafi ambapo amewataka wananchi na Wafanya biashara watupe taka taka katika maeneo husika.
" Hizi Dastibini tunazitoa kwa kumuandika mtu jina na kuchukua Mawasiliano yake na kumpa ya kwetu ili ikitokea wale wakaidi wa agizo la kutumia kinyuny Dastibini hizo watoe taarifa haraka kwa Viongozi na polisi Kata ili hatua za kisheria zichululiwe " Ameongeza DAS Sheila.
Naye Diwani wa Kata ya Gerezani, Fatuma Abubakari, amesema usafi ni muhimu bila usafi ongezeko la Magonjwa ya milipuko yataongezeka. Amewataka Wananchi kutii Sheria na kutolazimisha faini zisizo za kilazima.
Aidha Diwani huyo ametoa Shukrani za dhati kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh: Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Mh: Sophia Mjema, Katibu Tawala Sheila Edward na Uongozi mzima wa Manispaa ya Ilala hususani Idara ya Mazingira na Usafishaji kwa kuja na kampeni nzuri ya kuhamasisha Usafi.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Idara ya Mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda, amesema zoezi hilo wameriratibu kwa malengo mahususo kabisa ya kuweka Jiji safi .
Amesema kuwa shughuli ya usafi walianza kutoa Elimu lakini wakaja na mfumo wa kutoza faini kwa watu wanaokiuka utaratibu wa kisheria wa kuchafua Mazingira. "DAS Ilala apongeza jitihada za Manispaa Kitengo cha Usafishaji na Mazingira katika zoezi la ugawaji Dastibini Kata ya Gerezani.
"Hili ni zoezi endelevu kwani tulianza muda mrefu baada ya kupata tamko kwa Rais wetu John Magufuli lakini cha kushangaza wapo watu wanakupinga mfumo huu Sasa utaratibu wetu ni faini tuuu, tumeanza Kata ya Gerezani lakini tutavuka kila eneo kwakuwa tumejipanga kuona Mazingira katika Manispaa yetu yanakuwa safi na kuvutia" Amesema Mapunda.
Hata hivyo, Mapunda amesema kuwa lengo la usafi sio kumnyanyasa mtu na kumpiga faini Bali ni kuhakikisha Jiji Letu la Dar es Salaam linakuwa safi na kuongoza kwa Majiji yanayofanya vizuri Tanzania.
Miongoni Mwa wananchi waliokabidhiwa usimamizi wa Dastibini hizo, Baton Nyerema , ameupongeza Uongozi wa Manispaa Idara ya Usafishaji na Mazingira pamoja na Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema kwa kuja na mbinu mbadala ya kupunguza taka taka zinazo zagaa mitaani.
Amesema maeneo mengi yanakuwa machafu kwa kukosa vifaa vya kutupia taka wakati huo huo alienda mbali na kumshukuru Rais wa Tanzania Mh John Magufuli kwa kuanzisha kampeni ya usafi ambayo kwa kiasi kikubwa imeboresha mazingira na kupunguza Magonjwa ya milipuko.
Pia DAS Sheila , amewataka wafanya Biashara waache tabia ya kumwaga uchafu kwenye mitaro ya kupitisha maji ya mvua .
Hata hivyo amewataka Wafanya biashara walio karibu na matundu hayo wawe walinzi namba mmoja la sivyo wao watawajibika.
Katika hatua nyingine, Katibu Tawala Sheila Edward, amewataka wamiliki wa Magari wote hususani Dala dala kuweka Dastini ndani ili kupunguza uchafu na wanyunyize Dawa za kuulia wadudu ( Farmigation) kama kunguni kwenye Siti za Abiria maana tatizo hilo limekuwa likijitokeza Dala Dala nyingi hapa mjini
Post a Comment