TBF yawaomba Wazazi na Waalimu kuchangamkia fursa ya mafunzo ya Mpira wa Kikapu Nchini.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu hapa nchini, Phrase Magesa (Kushoto), akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya ufunguzi wa ligi ya NBL, kulia ni Kamishina wa ufundi na Uwendeshaji wa Mashindano TBF, Manasi Zabron.
SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu hapa nchini limewaomba Wazazi na Waalimu kuchangamkia fursa za mafunzo watakayo yatoa hivi karibuni katika kukuza mchezo huo.
Hayo yamezumgumwa Leo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu hapa nchini ( TBF), Ndugu Phrase Magesa, Mara baada ya ufunguzi wa Ligi ya mpira wa Kikapu Tanzania ( NBL) kumalizika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Rais TBF, Magesa, amesema wapo katika mchakato wa kuandaa mafunzo yatakayo Shirikisha ngazi Tatu za kitaaluma ikiwamo , Ukocha, Refalii pamoja na Mtunza Takwimu.
Aidha amesema kuwa, mafunzo hayo watayatoa kwa ngazi Tatu ikiwamo Walimu wenye uzoefu, wasio na uzoefu ( un professional) na wale walimuu wa Kimataifa ( Professional).
Pia amesema Mafunzo hayo yatafanyika nchi nzima kwa kuyagawa katika kanda 8 zikiwamo Kanda ya Zanzibar, Kanda ya Pwani, Kanda ya kati, Kanda ya Ziwa, Nyanda za huu Kusini, Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya kusini pamoja na Kanda ya Kaskazini. Amewataka Watanzania, Wapenda michezo , Waalimu na wadau wa Mpira wa Kikapu hapa nchini wachangamkie fursa hiyo Mara baada ya kutangaza mafunzo hayo.
" Tuna programu mbali mbali za Watoto zinazoendeshwa pala Kituo cha michezo cha Jk Youth Park chini ya Mwalimu Bahati Mgunda, lakini tumeona hii haitoshi kuutangaza mchezo huu hivyo maamuzi tuliyoyafikia ni kuandaa mafunzo haya nchi nzima ili mchezo huu uwe na tija kwa Taifa Letu na maisha ya Vijana wetu, tunao watoto waliofanikiwa kupitia mchezo huu kama vile Atiki mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya High View alipata nafasi ya kwenda Nairobi pia Jesca nae amezunguka Afrika Kusini , Senegal kupitia ligi ya NBA, hivyo wadau tunawaomba mjitokeze kupata fursa hiyo ya mafunzo tufike mbali " ,Amesema Rais Phrase Magesa.
Kadhalika amesemaamesema mchezo huo unafaida kubwa haswa za kielimu kwa Vijana wetu ambao ni Wanafunzi kwani wale wote wanafanya vizuri zaidi wanapata Scholarship.
Hata hivyo amesema licha ya mipango yao hiyo, bado kuna changamoto zinazo sababisha kuzorota kwa mchezo huo hapa nchini na kutofikia malengo pamoja na Chama na wanachama wake ambao ni Vilabu.
Miongoni Mwa changamoto hizo alizozitaja ni pamoja na Ufinyu wa Wadhamini ambapo unapelekea kudumaa kwa mchezo huo na baadhi ya timu kushindwa kusafiri na kufanya maandalizi, Suala la viingilio ambapo ukitangaza viingilio wadau wachache wanajitokeza jambo ambalo kama umewafukuza wasije uwanjani.
Hivyo ameomba Wadhamini wajitokeze kama walivyofanya Kiboko ambao udhamini wao unasaidia kuboresha miundombinu ya upakaji rangi Uwanja pamoja na Maji kwa Vilabu. Pia amesema kama Wadhamini wataongezeka, Hamasa ya mchezo huo utaongezeka, Wadhamini watajitangaza kupitia bidhaa zao na kukuza uchumi wa eneo husika kwa wafanya Biashara ndogo ndogo.
Amewataka wadau wa mikoani watoe ushirikiano kwa timu zao ili ziweze kusafiri. Naye Kamishina Ufundi na Uendeshaji wa Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu hapa nchini, Manas Zabroni, amesema uchache watimu kushiriki kutoka mikoani imetokana na baadhi ya timu kujitoa ikiwamo Bandari Tanga, Prisons Stars Wanawake na wanaume hii ni kutokana na uhaba wa fedha pamoja na Vilabu vingine kujikita katika michuoano ya Taifa Cup itakayotimua vumbi hivi karibuni katika kupata Timu ya Taifa.
Manasi amesema, Michuano hiyo ya NBL, yameshirikisha jumla ya Vilabu 8 upande wa Wanaume ambapo ni JKT , ABC, VIJANA, KURASINI HEAT, RUKWA STARS , SAVIO UKONGA KINGS pamoja na OILERS. Kwa upande wa Vilabu vya Wanawake jumla ni timu Tatu ikiwamo JKT STARS, DON BOSCO LIONESS na VIJANA QUERNS. Amesema ni timu moja pekee iliyotoka Mkoani hivyo kwa tafsiri ya haraka uchumi wa Vilabu umekuwa Mdogo na wengine nguvu zao wamejikita katika michuano ya Taifa Cup.
Aidha amesema kuwa katika Mashindano hayo wanategemea kuwa na washindi watatu, ambapo mshindi wa Kwanza na wapili watazawadiwa Kombe pamoja na Medali, huku mshindi wa Tatu atapatiwa Medali pekee.
Amesema kuwa mshindi wa kwanza na wapili watapata nafasi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika zone Namba tano. Amesema Nchi 11 zitapeleka washiriki katika Mashindano makubwa Lakini washindi wa wiwili ligi ya NBL watawakilisha Mashindano ya zone tano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki ambapo kwa Tanzania imepewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mashindano hayo .
" Haya ni Mashindano makubwa sana japo ni timu chache zimeshiriki lakini changamoto zipo hivyo tunaomba wadau na Baraza la Michezo Tanzania ( BMT) liweze kutusaidia sana kuutangaza mchezo huu licha ya kuwa wapo baadhi ya Wadhamini lakini haitoshi tunaandaa ligi hii katika mazingira magumu" Amesema Manasi.
Amesema zipo changamoto kama vile kulipa waamuzi , kukodi Uwanja , gharama ya umeme pamoja na mafuta ya Jenereta ya akiba.
Mwalimu wa Oilers , Lusekelo Mbwele, amesema Mashindano ni magumu lakini wamejipanga kushinda licha ya mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Ukonga Kings kuibuka na ushindi wa jumla ya Vikapu 63 kwa 52. Hata hivyo Mwalimu wa Ukonga Kings , Denis , Amesema Wadhamini changamoto kwani hawana vitendea kazi, gharama kusafirisha timu .
Katika ufunguzi huo, tulishuhudia Timu ya Jkt ikiibuka na Vikapu 87 kwa 54 dhidi ya Kurasini Heat.
Post a Comment