Header Ads

DC MJEMA AWATAKA WATENDAJI KWENDA NA KASI YA RAIS MAGUFULI.







MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amewataka Watendaji watoke kusikiliza kero za Wananchi badala ya kukaa Ofisini kuzungusha viti. Hayo ameyasema Leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam wakati wa Mjumuisho ya Ziara zake kwenye Majimbo matatu yakiwamo Ukonga, Segerea pamoja na Ilala.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari, DC Mjema, amesema Watendaji wanapoletewa kero mezani wanatakiwa wahakikishe wanazitatua.

 Amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano haitaji  Watendaji wazembe inataka  Watendaji wachapa kazi.

Amesema kero nyingi zinatokana na baadhi ya Watendaji kutowajibika hivyo kusababisha mrundikano wa kero .

 Aidha amewataka  Wakuu wa Idara kuhakikisha kwamba wanaweza kutatua kero na watumie muda wao Mwingi wa kutoka nje kutafuta changamoto.

" Watendaji mnatakiwa kutoka nje , mbona Mimi naweza kutoka Sasa acheni uzembe huu ni muda wa kufanya kazi sio muda wa Maneno yasiyo na mujibu, Viongozi wazuri wanaonekana kwa uchapakazi wao hivyo wakuu wa Idara sitaki masihala atakaeshindwa kutatua kero nakuomba Mkurugenzi lala nao mbele tunataka  Ilala yenye maendeleo lakini tuwe na hati safi " Amesema DC Mjema.

 Pia DC Mjema amewataka Watendaji kufanya kazi Massa 24 ili wahakikishe kila MTU anapofika Ofisini kero yake inapatiwa ufumbuzi sio kila siku kumrudisha mwananchi njoo kesho hilo katika Ilala hii hawezi kulivumilia.

Amesema mwisho wa kufanya kazi sio masaa nane kama walivyozoea badala yake watoke kuangalia changamoto nje ya ofisi zao huku akimwagiza Mkurugenzi kufungia viti Store kwa Watendaji wasio toka nje.

 Amesema Katika ziara zake yapo mambo yaliyo patiwa majawabu na mengine kufikisha katika Wizara husika huku mengine wakiyakabidhi kwa TAKUKURU kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

 Amesema kuhusu kero ya Maji, amegundua kwamba Wananchi hawapatiwi mapato na matuminzi kutoka kamati za Maji hivyo amewaagiza wa husika na Watendaji kuwajibika katika hilo.

Amewataka watu wa DAWASA watakapo maliza mradi yao wasambaze Maji haraka ili Wananchi wapate huduma hiyo kwa haraka na kuondoa kero hiyo.

 Katika mikopo, DC Mjema, ameitaka Manispaa kupitia Afisa maendeleo waharakishe uratibu wao haraka ili Pesa hizo ziwafikie wahusika  licha ya hapo amewaagiza Afisa maendeleo wa kata wa kuhakikisha atakapotembelea tena kata hizo wafikie nusu ya uratibu wa Vikundi ili Pesa zikotoka zikatumike kwa walengwa.

 " Hili zoezi lipo chini kuna baadhi hamuwajibiki nasikia mpaka Leo hili zoezi linayumba sasa Maafisa Maendeleo hakikisheni nitakapo rudi tena mtaa kwa mtaa muwe mmefikia kati kati ya kuratibu Vikundi hivyo" Ameongeza DC Mjema.

Kuhusu huduma za Afya, DC Mjema, amesema Bahari Pharmacy yupo kwa ajili ya kuhudumia mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuhakikisha huduma za Dawa katika vituo vyetu vya Afya zinapatikana  na kusambazwa kila kona ya Manispaa na mkoa kwa ujumla.

GKuhusu Wazee  kutopatiwa Dawa za Magonjwa yasiyoambukizwa kwenye vituo vya Afya, amemuagiza DMO alifanyie kazi hilo ili wazee wapatiwe huduma hizo .

pia ametoa kalipio Kali kwa wauguzi wenye  kauli chafu kwa Wagonjwa na wala rushwa  huku akimtaka Mkurugenzi kuwatimua kazi Mara moja.

Katika hatua nyingine, amemuagiza Mkurugenzi kuongea na Afisa Ushirika na mujibu hoja za kwanini amekuwa akilazimishwa kufanya kazi za ziara ambapo tangia ziara zianze kazi yake amekuwa ni kuagiza watu tuu.

 Amesema Afisa Ushirika lazima atoke ofisini ili kutatua kero za nje za Wananchi kwani kero nyingi zipo kwenye masoko na Taasisi za Biashara.

Upande wa TASAF, Amesema Viongozi wanaowaandikisha Vijana wao Dawa yao IPO jikoni kwani TASAF ipo  kwa ajili ya Wazee tuu sio Vijana.

 Soko la  Feri Kivukoni amesema tayari ametengeneza Jopo lake kuhakikisha matatizo ya Zone zote yanapatiwa ufumbuzi ikiwamo ukarabati wa Soko hilo.

 Kuhusu ardhi amesema amegundua kwamba ipo  migogoro ya watu kuvamia eneo, watu kutolipwa stahiki zao na wengine kulipwa stahiki lakini bado hawaondoki na baadhi ya Watendaji kujihusisha na uuzwaji wa maeneo zaidi ya watu wawili.


Amewataka Watendaji kuwa makini wakati wa urasimishaji wa ardhi katika kamati zao. Katika kuhitimisha hayo, amesema kero zitakazo mfikia yeye atampatia  DAS kuwaandikia kero hizo Idara husika na kama watashindwa Mkurugenzi atawachukulia hatua.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.