Manispaa ya Ilala kutoa Bajaji 30 kwa Vijana.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri, amesema wamejipanga kutoa Bajaji 30 kwa Vijana kama mikopo katika kuwawezesha kiuchumi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mjumuisho wa ziara ya DC Mjema Leo, amesema mpaka sasa Manispaa yake imetenga Shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya kuwezesha huduma za Kijamii katika kuleta maendeleo.
Amesema Vijana wengi wamekuwa katika changamoto kubwa kutokana na Soko la ajira kuwa Dogo hivyo wakiwakopesha watakuwa wamewasaidia kwa kiasi kikubwa sana kujikimu na kupambana na umasikini.
Aidha, amesema Serikali ya awamu ya tano imekuja na mikopo ya 10% kwa wakina Mama, Vijana na Walemavu lengo ni kufanya jamii iwe ya kujitegemea na mikopo hiyo haina riba.
" Sisi kama Manispaa tumejikita kuhakikisha kwamba mikopo inatolewa na hizi Bajaji tutazitoa kwa utaratibu Mwalimu japo zinaonekana chache lakini zoezi hilo litakuwa endelevu lakini wataongeza uhitaji kadri wateja watakavyokuwa waaminifu Katika urudishwaji wa mikopo" Amesema Mkurugenzi.
Hata hivyo, amesema Bajaji hizo zitatolewa katika makundi amewataka maafisa maendeleo wa Kata kuhakikisha wanaratibu zoezi hilo ili wakianza utaratibu wa kugawa hizo Bajaji ziwafikie walengwa kama ilivyokusudiwa.
Amesema bado ajira ni tatizo kwa Vijana hivyo amewataka wajikite katika kujiajiri badala ya kufikiria kuajiriwa kwani Serikali imekuja na kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda na waibebe ili tuweze kufikia katika uchumi wa kati.
Licha ya kupunguza wimbi la ajira lakini watapunguza uharifu kutokana na Vijana watakuwa na ajira na watashindwa kujiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani kama vile kuiba, ubakaji, uporaji pamoja na uharifu wa silaha.
Post a Comment