DC Mjema awataka Wakuu wa Idara Watendaji, wafanye kazi wasioweza wakae pembeni
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesaini makubaliano na Wakuu wa Idara wa Manispaa Ilala kwa ajili ya kushughulikia kero zinazotolewa na wananchi kwenye idara zao, na kwamba wasipozishughulikia watatakiwa kutoa maelezo.
Mjema alisema jumla ya kero 2,265 ambazo wamezisikiliza katika Kata 36 za manispaa hiyo, zinaweza kutatuliwa na wakuu wa idara, watendaji wa Kata na mitaa na kwamba wasikwepe majukumu yao.
"Manispaa imelenga kukusanya mapato ya Sh bilioni 56 kwa mwaka kwa kuendelea kuboresha masoko, machinjio, machinga na stendi ya kisasa ya Chanika"alisema Mjema
Akitoa majumuisho ya ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi Dar es Salaam, alisema kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika sekta ya ardhi, afya, maji, masoko na mikopo.
Mjema alisema mara nyingi watendaji na wakuu wa idara wamekuwa wakikwepa kutatua kero kwa madai kuwa kero hizo haziwahusu, na kuwataka wananchi kuwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya, licha ya kwamba wanauwezo wa kuzitatua.
"Katika hii fomu kila mkuu wa Idara atapewa kero tulizokutana nazo wakati wa ziara, atatakiwa kuzishughulikia kwani ifikapo Desemba mwaka huu tutakutana hapa na tutaelezana kero zilizokwisha na zile ambazo hazijafanyiwa kazi mtatoa maelezo kwanini mmeshindwa," alisema .
Alisisitiza kuwa viongozi watakaoona kwamba hawawezi kuendana na kasi hiyo, kwa kuwasikiliza wananchi, kutatua kero zao pamoja na kutotimiza majukumu yao ipasavyo, wajitoe wakafanye kazi nyingine kabla ya kusimamishwa kazi.
Alieleza kuwa wananchi wengi hawasikilizwi kero zao na kwamba kero kubwa waliyokutana nayo ni migogoro ya ardhi.
Alifafanua kuwa viongozi wa mitaa na Kata wamekuwa chanzo cha migogo hiyo kwa kuwasaidia wavamizi kuchukua maeneo ya wananchi ambapo wamekuwa wakiwagongea mihuli ilhali wanafahamu kuwa sio maeneo yao.
Mjema alisema viwanja 222 vilivyopo eneo la viwanja vya ndege vimetengwa kwa ajili ya huduma za jamii na kwamba wananchi wanatakiwa kulipwa fidia, lakini viwanja 272 havijulikani vilipo.
Alieleza kuwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) inapaswa kumaliza taharuki kwenye viwanja 514 vilivyopo eneo hilo ili wananchi wajue hatma ya maeneo hayo.
Aidha, ameagiza fedha zilizokusanywa na wananchi kwa ajili ya kufanya urasimishaji ambazo zilitakiwa kulipwa kwa kampuni ya kupima viwanja ambayo haikupitishwa na halmashauri hiyo, ili wananchi wachague ni mtu gani atawafanyia upimaji wa viwanja.
Kwa upande wake, Mkurugenz wa Manispaa hiyo, Jumanne Shauri alisema kuwa malengo ya manispaa hiyo ni kudumisha amani, utawala bora na kufikia maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2020.
Alisema wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaongeza mapato kufikia bilioni 56 ifikapo Juni 2019 kwa kupitia masoko, vyanzo vipya vya mapato na uboreshaji wa machinjioni ya Vingunguti.
"Ujenzi wa soko la Vingunguti tumetenga Sh bilioni 13.4 na likikamilika tunategemea kukusanya Sh bilioni tatu kwa mwaka, machinjio ya Vingunguti yatasaidia kuongeza mapato na ajira pamoja na masoko yetu 35 yatafanyiwa ukarabati kwani yameajiri zaidi ya watu 8,000 hivyo tunaamini tutaongeza mapato Turkish a yak Amravati," alieleza Shauri.
Alisema stendi ya kisasa itakayojengwa Chanika imetengewa Sh milioni 190 na kwamba itakapokamilika itaingiza Sh milioni 600 kwa mwaka.
Shauri alisema kutakuwa na mfumo wa teknolojia kwa ajili ya kukusanya mapato na kwamba wanaamini fedha hiyo itakapokusanywa itasaidia miradi ya maendeleo kutekelezwa.
Aidha, alisema wanatarajia kujenga hospitali ya kisasa maeneo ya Kivule na kwamba tayari Sh milioni 500 zimewekwa kwenye akaunti na serikali huku manispaa hiyo ikiwa imetenga Sh milioni 250.
"Hospitali hii itakapokamilika itasaidia kupunguza msongamano katika hospitality zetu, pia tumejidhatiti katika suala la ununuzi wa dawa kwenye hospitali zetu.. Eneo la Vingunguti kwa Mnyamani tutajenga kituo cha afya tumetenga Sh milioni 500 kwa ajili ya kununua maeneo yatakayozunguka kituo hicho ili kuongeza nafasi..
Mkurugenzi huyo alisema wametenga Sh milioni 600 kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji kwa wakazi wanaoishi pembezoni kwa wilaya hiyo ikiwemo Kata za Kinyerezi, Bonyokwa na maeneo mengine.
Pia alisema katika suala la mikopo, watanunua bajaji kwa ajili ya kuwapatia vijana watakaokuwa kwenye vikundi ili wawakopeshe na kisha kufanya marejesho.
Post a Comment