DIWANI WA KATA YA ILALA AWAPONGEZA WALIMU NA WANAFUNZI WA BENJAMIN W. MKAPA KWA UMOJA NA MSHIKAMANO
Diwani wa Kata ya Ilala ,Mhe Saady Khimji, leo alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Kidato cha nne kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa High School.
Mahafali hiyo ilifanyika katika viwanja vya Shule hiyo iliyopo maeneo ya Karibu na Shule ya Uhuru Mchanganyiko.
Katika Mahafali hiyo Wanafunzi wanaohitimu walifanya maonyesho mbalimbali ambayo ilipelekea Mgeni Rasmi na waalikwa wote kukiri vipaji vilivyopo, kulikuwa na maonyesho ya Ukakamavu yalionyeshwa na Skauti wa hapo Shuleni, Wimbo wa Taifa wa China ulioimbwa vyema kabisa na Mmoja wa wanafunzi wanaojifunza Kichina shule hapo, Igizo, Shairi na uimbaji wa nyimbo ya kuaga kwa wanafunzi wanaomaliza shule hivi karibu, aidha kulikuwa na Vijana walioonyesha Fashion show kwa mitindo mbalimbali bila kusaau Vijana waliocheza Dancer kwa umaridadi mkubwa.
Kupitia Mahafali hiyo Changamoto na Mafanikio mbalimbali yalielezwa tangu kuanzishwa kwa Shule hiyo Rasmi Mwaka 1999.
Sehemu ya Changamoto hizo ni kama hizi zifuatazo:-
1. Ukosefu wa Maktaba.
2. Uhaba wa Vifaa vya Maabara, Vitabu vya Kiada na Ziada.
3. Ukosefu wa Vifaa vya Michezo kama Jezi, Mipira, Sox na kadhalika.
4. Upungufu wa Walimu wa Masomo ya Accountancy na Mathematics.
5. Ukosefu wa Uwanja wa Basket Ball na Netball.
6. Ukosefu ma maeneo maalum ya kujisomea kwa pamoja (Vimbweta).
7. Ukosefu wa Ukumbi wa Mikutano na Shughuli nyinginezo Shuleni.
8. Ukosefu wa Usafiri Maalum hapo Shuleni.. n.k.
Ikumbukwe Shule hiyo ya Benjamin Mkapa inawafunzi Mchanganyiko, wapo Wanafunzi walemavu Ngozi, Wapo walemavu wa Uziwi, wapo wenye uono mdogo, wapo mabubu na wenye ulemavu wa Viungo.
Katika Mazingira hayo juhudi kubwa zimekuwa zinafanywa na walimu pamoja na wanafunzi kuhakikisha Shule inafanya vyema wakati wote.
Kipekee Mkuu wa Shule Madame Saria alimshukuru Mkurugenzi wa Jiji kwa kuwawezesha Madarasa 7 ya kujifunzia na Ofisi Moja ya Walimu, Shule ina wanafunzi 1640 na Walimu 114.
Aidha Mkuu wa Shule alimpongeza Mhe *Rais John Pombe Magufuli* kwa kazi nzuri anayoifanya na haswa katika Sekta ya Elimu.
Katika maelezo yake Mgeni rasmi aliwapongeza Walimu na Wanafunzi walioandaa Mahafali hiyo hakika ilikuwa Mahafali ya Kipekee kabisa Mkoa Dsm.
*"Nawashukuru sana Walimu kwa kunialika kuwa Mgeni Rasmi katika hafla kubwa na kipekee Shuleni hapa, Madiwani tupo wengi kitendo cha kuniona nafaa zaidi kuwa Mgeni Rasmi ni heshima kubwa kwangu, familia yangu, wananchi wenzangu Kata ya Ilala na Wana Dsm kwa ujumla, nimekuja hapa leo nikiwa na baraka zote za Mbunge wetu Mhe Mussa Azzan Zungu*, nimekuwa nikiwasiliana nae siku hizi mbili akiwa na hamu kubwa nimuwakilishe katika kusikiliza na hatimaye kuzichukua na kumuwasilishia Changamoto zilizopo Shuleni hapo, Mhe Mbunge yupo pamoja nasi ijapo yupo kwenye Majukumu ya Kibunge Mkoa wa Dodoma, anawasalimu sana na kuwapingeza wahitimu wote".
Aidha Katika kuunga Mkono maendeleo ya Shuleni hapo Diwani Khimji Alichangia Jezi seti moja na mpira moja kwa niaba ya Mhe Mbunge Zungu, lakini pia aliongoza harambee fupi kwa kuanza kuchangia yeye mwenyewe ili kutunisha mfuko wa Kamati ya Maandalizi ya Mahafali hiyo.
Mwisho Mgeni rasmi Mhe Saady Khimji aligawa vyeti vya kuhitimu kwa Wanafunzi wote 264 wanaohitimu hivi karibuni.
*MUNGU IBARIKI BENJAMIN MKAPA MUNGU IBARIKI TANZANIA.*
Elimu ni Ufunguo wa Maisha wazazi wekezen
Post a Comment