Header Ads

Naibu meya ilala atoa salamu za rambi rambi kijana aliyedondokewa na ukuta Ukonga

Naibu  Meya  wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya vingunguti, Omary Kumbilamoto, ametoa salamu za rambi rambi kwa familia iliyompoteza kijana ajulikanaye kwa jina la majuto masinga mara baada ya kuangukiwa na ukuta na kufariki.
Naibu meya ilala atoa salamu za rambi rambi kijana aliyedondokewa na ukuta Ukonga
katika ziara hiyo, Mh kumbilamoto aliambatana na diwani wa kata ya ukonga , Mh: mwaipopo pamoja na uongozi wa serikali ya mtaa wa markazi na kufanikiwa kutembelea eneo ambalo tukio hilo lilitokea hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mh kumbilamoto, alitoa salamu hizo huku akiwapa pole wote walioguswa na msiba ndugu, jamaa pamoja na marafiki wa karibu wa marehemu majuto.

Alisema kuwa, kila umma utaonja umauti lakini alifafanua zaidi akisema mwenyezi mungu kamuandikia binadamu kifo muda na wakati wake hivyo kama mtu ikifikia siku yake ya kufa basi mwenyezi mungu atachukua kiumbe chake alichokiumba.
Image result for omary kumbi lamoto"Nipende kuwaomba wale wote walioguswa na msiba huu ikiwamo  ndugu wa familia kuwa na subira katika kipindi hiki kifupi kigumu kwani hata mimi  msiba huu umenigusa sana ukizingatia kijana bado mdogo pengine alikuwa na ndoto za kufanyia makubwa familia yake na taifa kwa ujumla"alisema kumbilamoto. 

Katika hatua nyingine, diwani wa kata ya ukonga, Mh mwaipopo, alisema  kuwa ukuta huo ulikuwa na ufa hivyo kwa mujibu wa watu wa karibu waliokuwa wakimwambia mwenye nyumba kuhusu ufa yeye alikuwa mkaidi huku akisema jambo hilo sio la kweli .

Aidha, ndugu wa marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema msiba huo ulitokea ambapo kijana wao alikuwa kwa kaka yake na kwa sasa msiba umehamia kwa baba yake mkubwa ambapo mwili wa marehemu uliokuwa muhimbili unatarajia kusafirishwa kwenda mkoani dodoma mara baada ya taratibu zote kukamilika.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.