HALMASHAURI KUU YA CCM WILAYA YA MOROGORO MJINI YAFANYA KIKAO CHA KUPOKEA NA KURIDHIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Morogoro Mjini wamepokea na kuridhia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023-2024 na mipango ya mwaka wa fedha 2024-2025.
Kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ,kimefanyika Desemba 14-2024 huku kikijumuisha wataalamu mbalimbali kutoka Idara za Taasisi mbalimbali za Serikali kwa ajili ya kuwasilisha taarifa za utekelezaji za miradi ya maendeleo.
Kikao hicho kimekuwa na lengo la kusomewa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM
Akisoma taarifa ya utekelezaji, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Mussa Kilakala, amesema Manispaa ya Morogoro kwa mwaka wa fedha 2024/2025 imeidhinisha Bilioni 80,835,104,335.00 ambapo kwa mapato ya ndani imekadiria kukusanya Bilioni 15,562,887,000.00 ambapo matumizi ya kawaida ni Bilioni 68,304,541,000,.00 na ruzuku ya miradi ya maendeleo Bilioni 10,022,240,854.97 .
DC Kilakala,amesema hadi kufikia 30 Novemba 2024, jumla ya shilingi biloni 37,228,838,877.87 sawa na asilimia 46 lengo la mwaka zilikusanywa amabpo mapato ya ndani ni shilingi bilioni 4,951,200,634.83 sawa na asilimia 31.8 ambapo ruzuku ya kawaida ni shilingi bilioni 31,384,579,994.00 sawa na asilimia 46 na ruzuku ya miradi ya maendeleo ni shilingi bilioni 4,332,079,775.00 sawa na asilimia 43.
Hata hivyo DC Kilakala, amesema katika kufikia malengo, mafanikio ya Manispaa ya Morogoro ni matokeo ya vipaumbele vilivyowekwa kwenye MPANGO wa Maendeleo kwa lengo la kuendeleza na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi katika sekta za Afya, elimu, kilim, mifugo na ushirika, maji, barabara na mendeleo ya jamii kwa kushirikisha Wadau mbalimbali.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM ,Ndg. Fikiri Juma,ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao cha Halamshauri Kuu ya CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, ameipongeza Manispaa kwa kutekeleza vyema miradi ya maendeleo.
Fikiri,amesema zipo changamoto wameziona changamoto kadhaa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika ziara ya kamati ya siasa,hivyo changamoto hizo zikafanyiwe kazi.
Aidha,amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipa Manispaa ya Morogoro fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Post a Comment