Header Ads

MANISPAA YA MOROGORO YAADHIMISHA MIAKA 63 YA UHURU WA TANGANYIKA




MANISPAA ya Morogoro  imeadhimisha miaka 63  ya Uhuru  wa Tanganyika kwa kufanya mdahalo kuhusu maendeleo yaliyopatikana katika kipindi hicho.

Sherehe hizo za uhuru zimefanyika Desemba 09-2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro na kuhudhuriwa na wazee marufu pamoja na wananchi.

Akizungumza katika mdahalo huo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Mhe. Mussa Kilakala, amesema  kwa heshima ya mafanikio haya ya kihistoria, Serikali inafuatilia sekta zake kwa kutaja mafanikio yake, matatizo na changamoto ilizozikabili tangu Uhuru na kupanga mwelekeo wa baadaye.

Manispaa ya Morogoro imepata  mafanikio mbalimbali  ikiwemo sekta ya kilimo ambapo kipindi cha miaka 63 (1961-2024) Sekta ya  kilimo imekuwa na ongezoko la chakula cha kutosha huku uzalishaji wa kwa hekta kwa mazao imeongezeka ambapo tani 1 mwaka 2015/2016 hadi kufikia tani 2.3 mwaka 2023/2024 na uzalishaji wa mazao bustani uliongezeka kutoka tani 5 mwaka 2025/2016 hadi tani 16 mwaka 2023/2024.

Upande wa Sekta ya Viwanda, umeimarika kwa kushirikiana Serikali na Sekta binafsi ambapo mwaka 1961 hakukuwa na kiwanda kikubwa na vya kati na sasa 2024 viwanda vikubwa vipo 10, viwanda vya kati 5 na viwanda vidogo 452.

Sekta ya Umeme, mwaka 1961 maeneo mengi hayakuwa na umeme wa Gridi ya Taifa, ambapo katika kipindi cha miaka 63 maeneo mengi yamepatiwa umeme ambapo kwa Manispaa zaidi ya Mitaa 271 imesambazwa umeme.

Elimu ya Awali na Msingi, miaka ya 1975 Manispaa ya Morogoro ilikuwa na shule 8 za Serikali na mwaka 2024 ina jumla ya shule za Msingi 128 kati ya hizo Shule za Serikali ni 75 na binafsi ni 53.

Miundombinu ya madarasa, kwa mwaka 2024 madarasa yamejengwa 839 wakati mwaka 2019ilikuwa na vyumba 643 huku nyumba za waalimu mwaka 2019 zilikuwa 70 na sasa 2024 zipo nyumba 81,matundu ya vyoo mwaka 2019 yalikuwa 680 na mwaka 2024 yapo 972, madawati mwaka 2019 yalikuwa 14699  na mwaka 2024 yapo 16718 , waalimu shule za Msingi mwaka 2019 walikuwa 1401 na mwaka 2024 wapo waalimu 2019.

Upande wa Elimu Sekondari, mwaka 1961 zilikuwa sekondari 2 Kilakala na Morogoro Sekondari hakukuwa na shule binafsi na mwaka 2024 shule za Sekondari 60 ambapo 30 za Serikali na 30 shule binafsi,mashirika ya dini au Taasisi ,mwaka 1961 kulikuwa na wanafunzi 163 na mwaka 2024 wanafunzi wameongezeka kufikia 28476.

Sekta ya Maji,kutoka mwaka 1961 Manispaa ilikuwa inahudumiwa na chanzo kimoja cha maji kilichojulikana kwa jina la Mambogo ,kufikia mwaka 2024 maeneo mengi yanapata huduma ya maji ambapo Serikali imetoa fedha Bilioni 185 kwa MORUWASA kutekeleza mradi  wa mtambo mpya wa kuti u maji Mafiga,kuinua tuta katika Bwawa la Mindu pamoja na kutandaza mabomba makubwa.

Katika kuona changamoto ya maji inapungua ,Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan,imetoa fedha Bilioni 19.15  kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za maji eneo la Kihonda, Lukobe, Kiegea, Kilimanjaro, Viwandani, SGR na Mkundi kwa ujumla upo asilimia 95 na mradi huo utawanufaisha wananchi zaidi ya 135000.

Kwenye sekta ya barabara ,kipindi cha uhuru 1961 idadi ya kimometa za barabara zilikuwa chache na hazipitiki kirahisi na hakukuwa na barabara za lami ambapo katika kipindi cha miaka 63 kumejengwa kilometa 52.314 za barabara za Lami/Zege, kilometa 132.699 barabara za Changarawe,Kilometa 520.23 barabara za udongo,barabara za Wilaya na za Mitaa zimeendelea kuboreshwa ili ziweze kupitika kwa wakati wote ambapo kwa sasa kuna mradi mkubwa wa TACTIC unaojenga barabara kwa kiwango cha Lami katika Kata za Tungi, Kihonda na Mazimbu.

Huduma za Afya, mwaka 1961 Manispaa haikuwa na hata kituo kimoja cha kutolea huduma za afya, kwa sasa Manispaa ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 87 ambapo kuna Hospitali 4 vituo vya afya 14 na Zahanati 54 ,Kliniki 15 na Maternity home 1.

Upande wa Maliasili, Manispaa inalenga kuongeza maeneo ya kupanda miti  kwa kushirikiana na wadau wa mazingira ambapo mpaka sasa 2024 Manispaa imepanda zaidi ya miti 4,316,473.

Ufugaji, mwaka 1961 ufugaji ulikuwa hauna tija lakini kwa sasa mwaka 2024 Manispaa ya Morogoro imekuwa na miundombinu ya huduma za ufugaji ikiwemo Majosho 3, Lambo 1 na Machinjio 1  na kwa sasa Manispaa inatekeleza Mradi wa ujenzi wa Machinjio mpya na ya kisasa katika Kata ya Mkundi 

Sekya ya uvuvi ina jumla ya masoko 2 ya Samaki , mabwawa ya samaki 175,kutoa elimu ya ufugaji kwa zaidi ya watu 652.

Kwa mwaka 2020/2021 katika Sekta ya uvuvi,makusanyo ya mapato yalikuwa 72,357,500.00 hadi kufikia 2023/2024 makusanyo yalipanda kufikia 139,199,700.00

Manispaa ya Morogoro kabla ya mdahalo wa maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru, kuna michezo  mbalimbali ilifanyika kama vile mpira wa miguu,mpira wa pete,mchezo wa bao na mbio za pole ambapo wananchi mbalimbali walishiriki.

Mbali na michezo hiyo ,pia kulifanyika matukio mbalimbali ya Kijamii ikiwemo kufanya usafi maeneo yanazozunguka taaisisi za Serikali katika eneo la Kituo cha afya Mafiga pamoja na kufanya usafi wa mazingira ikiwemo upandaji wa miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mwisho DC Kilakala, amewasisitiza wananchi kutumia fursa zinazoendelea kujitokeza ili kupunguza umasikini na kuboresha hali ya maisha.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.